Pata taarifa kuu

Comoro: Hali ilivyo baada ya wito wa kufanya maandamano kutofuatwa na upinzani

Siku ya Ijumaa Januari 19 ilikuwa shwari mjini Moroni na pia kote nchini, licha ya wito uliotolewa na wagombea watano wa upinzani ambao wanabaini kwamba wameghadhabishwa kukutokana na matokeo ya uchaguzi wa urais.

Mwanasiasa wa upinzani Daoudou Abdallah Mohamed, mgombea wa chama cha Orange, amewasilisha malalamiko yake katika Mahakama ya Juu ya Moroni, huko Comoro, Jumamosi hii, Januari 20, 2024.
Mwanasiasa wa upinzani Daoudou Abdallah Mohamed, mgombea wa chama cha Orange, amewasilisha malalamiko yake katika Mahakama ya Juu ya Moroni, huko Comoro, Jumamosi hii, Januari 20, 2024. © David Baché / RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwandishi wetu maalum, David Baché na mwandishi wetu wa Moroni, Abdallah Mzemba

Baada ya kuchaguliwa tena kwa Azali Assoumani, ghasia zilizuka mjini Moroni na wagombea watano wa upinzani wakaitisha, bila vurugu, kuunga mkono maandamano, lakini wito wao haukufuatwa. Kando na mikusanyiko michache midogo, hakuna maandamano makubwa yaliyofanyika, iwe katika mji mkuu wala kwingineko nchini. Hata hivyo, kambi ya rais na ile ya upinzani hawachukulii sawa matokeo ya uchaguzi wa urais.

Waliitisha maandamano katika "miji na vijiji" vya nchi, na "kuingia mitaani", baada ya sala ya Ijumaa. Hata hivyo, hakuna maandamano yaliyoripotiwa nchini humo.

Daoudou Abdallah Mohamed, kutoka chama cha Orange, ni mmoja wa wagombea watano wa upinzani waliotitisja maandamano hayo: "Jambo muhimu zaidi ni kwamba jana [Ijumaa Januari 19] ilikuwa siku ya maombi ya kumbukumbu ya kijana huyu [aliyeuawa kwa risasi siku mbili za ghasia] na kulaani matumizi ya nguvu kupita kiasi. Ilikuwa siku ya sala. Sio wote walikuja kutoka Moroni na kila mtu alisali nyumbani kwake. "

Houmed Msaidié, msemaji wa serikali na mkurugenzi wa kampeni wa Rais Azali Assoumani anaona mambo kwa njia tofauti: "Watu kamwe hawaitikii mwito wao wa kuandamana. Nchi inaendelea na shughuli zake. Watu wa Comoro hawako tayari kusikiliza wito wao usiojenga. Ingekuwa bora marafiki zetu wagombea wangeazimia kutoa malalamiko yao kwa taasisi za kisheria badala ya kuendelea kutoa wito usiotikiwa. "

Siku ya Ijumaa hii asubuhi, wagombea wawili kati ya watano wa upinzani waliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu ili kupata ubatilishaji wa uchaguzi wa urais. Na mgombea wa tatu anapanga kufanya hivyo mwanzoni mwa wiki ijayo. Chama cha rais aliyechaguliwa tena, Azali Assoumani, pia kimeatangaza kwamba kimewasilisha rufaa, kikibaini kwamba kiwango cha ushiriki kilikuwa 60% na sio 16%, hali ambayo, kwa kweli, inatilia shaka matokeo ya uchaguzi.

"Tumechagua kutumia njia zote zinazowezekana za kisheria. Amani, utulivu wa nchi hii upo katika jengo hili, Mahakama ya Juu. Maana leo tumetoa ushahidi wote, " amesema Daoudou Abdallah Mohamed, mgombea wa chama cha Orange

Hali nchini humo inatia wasiwasi Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Uhuru nchini Comoro, ambayo ilichapisha taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumamosi. CNDHL huanza kwa kuwataka raia, Serikali na watendaji wa kisiasa "kujizuia. "

Ingawa hali ya utulivu imerejea tangu Ijumaa, siku za awali zilikuwa na matukio ya vurugu. Majengo kadhaa ya umma na ya kibinafsi yalichomwa moto au kuporwa, maafisa wa serikali kushambuliwa na afisa wa polisi kupigwa. Kwa hivyo CNDH inasisitiza juu ya "haja ya kudumisha utulivu wa umma. "

Mmoja wa waandamanaji alipigwa risasi na kuuawa, na wengine kadhaa pia walipigwa risasi na kujeruhiwa. Juu ya "matukio haya ya kusikitisha" yote, CNDH "inataka kufunguliwa kwa uchunguzi wa mahakama", ili kila mmoja ahukumiwe kwa kile alichokifanya. Hatimaye, watu wengi walikamatwa. 

Hakuna takwimu rasmi zilizowasilishwa lakini angalau wapinzani wawili wa kisiasa na pengine makumi kadhaa ya waandamanaji vijana wanazuiliwa kwa sasa. CNDH inakumbusha kwamba kamata kama lazima ifanyike "kwa heshima kubwa kwa mfumo wa kisheria na utu wa binadamu" na kwamba "kila mtu aliye kizuizini ana haki. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.