Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais nchini Comoro: Washington yaomba kuwepo na uwazi

"Tunatoa wito kwa CENI na mamlaka ya Comoro kuhakikisha uwazi kamili na kufafanua matokeo yaliyotangazwa," ubalozi wa Marekani nchini Comoro umetangaza.

Kisiwa cha Anjouan, Comoro.
Kisiwa cha Anjouan, Comoro. CC BY-SA 3.0/Haryamouji/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

 

, Azali Assoumani, mwanajeshi wa zamani mwenye umri wa miaka 65 alichaguliwa tena kufuatia duru ya kwanza ya upigaji kura siku ya Jumapili kwa 62.97% ya kura lakini ushiriki ulifikia kiwango cha 16.30% tu, kulingana na takwimu rasmi zilizotangazwa siku ya Jumanne jioni na tume ya uchaguzi (CENI). Ushindi huu unapaswa kumruhusu kurejea kwa muhula wa tatu mfululizo na kusalia madarakani hadi mwaka 2029 katika visiwa hivi vya Bahari ya Hindi.

Upinzani, unaotaka uchaguzi ufutiliwe mbali, umelaani "udanganyifu mkubwa" na "kujazwa kwa masanduku ya kura". . Ubalozi wa Marekani ukibainisha "baadhi ya dosari zilizorekodiwa", umesisitiza kuwa matokeo "yameibua wasiwasi mkubwa ambao lazima ushughulikiwe ili kudumisha amani na ustawi wa taifa".

Matokeo ya uchaguzi yataidhinishwe katika siku zijazo na Mahakama ya Katiba, mahakama ya juu zaidi katika visiwa vya wakaazi 870,000, 45% kati yao ambao wanaishi chini ya mstari wa umaskini. Wananchi wa Comoro walipiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais wao lakini pia kuwachagua magavana wa visiwa vitatu vinavyounda Visiwa vya Comoro: Grande-Comore, Anjouan na Mohéli. Mojawapo ya mambo ya kuzingatia ni tofauti isiyotarajiwa ya takwimu za ushiriki katika chaguzi mbili zilizofanyika kwa wakati mmoja.

Kulingana na hesabu rasmi, Wacomoro 189,497 walipiga kura kwa uchaguzi wa magavana, lakini ni 55,258 pekee waliopiga kura kuchagua rais wao. "Tofauti ambayo haikuonekana kwa waangalizi wa kitaifa na kimataifa," unasisitiza ubalozi wa Marekani.

Mji mkuu wa Comoro ulikumbwa na makabiliano siku ya Jumatano na Alhamisi kati ya makundi ya vijana waliokuwa wakirusha mawe na polisi kujibu kwa mabomu ya machozi. Majengo yaliharibiwa na kuchomwa moto. Mtu mmoja aliuawa na sita kujeruhiwa, kulingana na idara ya huduma za dharura ya hospitali ya Moroni.

Sheria ya kutotoka nje usiku iilitangazwa tangu Jumatano hadi tarehe ambayo haijabainishwa. Watu kadhaa walikamatwa lakini hakuna takwimu zilizowasilishwa. Upinzani ulikuwa umeitisha "siku ya kitaifa ya maandamano" siku ya Ijumaa lakini mitaa ya Moroni, chini ya uangalizi mkali wa polisi, ilisalia katika hali ya utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.