Pata taarifa kuu

Asubuhi tulivu Moroni, siku moja baada ya wito kutoka kwa upinzani kuandamana

Nchini Comoro, siku tatu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais, upinzani ulitoa wito kwa watu kuandamana Januari 19, 2024. Siku moja baada ya makabiliano yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja, hali ilionekana kuwa shwari huko Moroni, mji mkuu wa nchi hiyo, saa sita mchana.

Waumini wakisaali, huku afisa wa polisi wa manispaa akiwa imara kukabiliana na maandamano yoyote yanayoweza kutokea, Januari 19, 2024 huko Moroni, siku ambayo wagombea watano wa upinzani waliitisha maandamano.
Waumini wakisaali, huku afisa wa polisi wa manispaa akiwa imara kukabiliana na maandamano yoyote yanayoweza kutokea, Januari 19, 2024 huko Moroni, siku ambayo wagombea watano wa upinzani waliitisha maandamano. © David Baché/RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwandishi wetu maalum huko Moroni, David Baché

Siku mpya ya uhamasishaji Ijumaa hii, Januari 19, 2024 nchini Comoro. Mikutano ya hadhara inapangwa kwa vyovyote vile kwa wito wa upinzani. Wagombea watano, ambao wanahisi waliibiwa kura baada ya kuchaguliwa tena kwa Rais anayemaliza muda wake Azali Assoumani, wanataka kupanua vuguvugu lililoanzishwa na vijana mara tu matokeo rasmi yalipotangazwa siku ya Jumanne Januari 16.

Lakini leo Ijumaa, saa sita mchana, angalizo ni kwamba watu walikuja kusali na wakarudi zao makwao. Mbele ya msikiti katika wilaya ya Badjanani, ambako RFI ilikwenda, katikati ya Moroni, baada ya sala, waumini walienda nyumbani, au walikaa kuzungumza na marafiki, lakini hakuna maandamano, hakuna mkusanyiko wa kudai chochote.

 

Watu wengi waliohojiwa wana maoni tofauti juu ya matokeo ya uchaguzi: baadhi wanamuunga mkono Rais Azali Assoumani, wengine wanajijizuia kuzumza chochote wakikumbusha kuwa kuna taasisi, na wengine wanasema wamechoshwa na udanganyifu huo, na "wizi wa kura kutoka kwa Wacomori."

Lakini mwito wa wagombea watano wa upinzani wa kufanyika kwa maandamano makubwa haukufuatwa. Je, watu waliogopa uwezekano wa kukandamizwa na polisi au jeshi? Hivi ndivyo wengine wanasema. Raia wa Comoro wamekumbusha kwamba kijana muandamanaji alipigwa risasi na kuuawa juzi, kifo ambacho lazima kikatishe tamaa.

Mtu ambaye hakufurahishwa na matokeo ya uchaguzi alieleza kuwa katika Ijumaa hii ya sala, hakuja kwa ajili hiyo.

Mahali pengine, katika mji mkuu, kulingana na maoni ambayo RFI iliweza kupata, uchunguzi unafanana: hakuna hata mmoja wa wagombea watano wa upinzani ambao walikuwa wameitisha maandamano aliingia mtaani huko Moroni. Wengine wako nje ya mji mkuu, katika maeneo wanakotoka. Lakini hata huko, katika hatua hii kwa hali yoyote, hakuna mikusanyiko au maandamano yanayoripotiwa. Utulivu unaotofautiana sana na mvutano wa siku mbili zilizopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.