Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Uchaguzi wa urais uliopingwa nchini Comoro: Sheria ya kutotoka nje imetangazwa

Sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa Jumatano kwenye visiwa vya Comoro, baada ya makabiliano kati ya waandamanaji na polisi katika mji mkuu, siku moja baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi Azali Assoumani katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliyogubikwa "udanganyifu" , kwa mujibu wa upinzani.

Wacomoro waliweka vizuizi katika vitongoji kadhaa vya mji mkuu, hasa huko Hamramba, kusini mwa Moroni, Januari 17, 2024.
Wacomoro waliweka vizuizi katika vitongoji kadhaa vya mji mkuu, hasa huko Hamramba, kusini mwa Moroni, Januari 17, 2024. © David Baché / RFI
Matangazo ya kibiashara

 

"Sheria ya kutotoka nje imetangazwa," mjumbe katika wizara ya Ulinzi Youssoufa Mohamed Ali ametangaza kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumatano jioni. Kulingana na sheria iliyochapishwa mara moja, hatua itakayoanza kutumika mara moja inaweka Moroni chini ya amri ya kutotoka nje kati ya moja usiku na saa kumi na mbili asubuhi, pamoja na maeneo mengine kati ya saa nne usiku na saa kumi na mbili asubuhi.

Siku nzima, katika mitaa ya Moroni, vizuizi vya barabarani vilivyotengenezwa kwa vipande vya lami, mawe na vifaa vya nyumbani viliwekwa barabarani. Biashara nyingi zilibaki zimefungwa. Majengo kadhaa yalichomwa moto, waandishi wa habari wa AFP wamebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.