Pata taarifa kuu

Comoros: Wagombea wa upinzani wanataka matokeo ya urais kutupiliwa mbali

Nairobi – Viongozi wa upinzani katika visiwa vya Comoros wanataka matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliopita kutupilia mbali.

Msemaji wa serikali Houmed Msaidie, ametuhumu upinzani kwa kupanga maandamano hayo
Msemaji wa serikali Houmed Msaidie, ametuhumu upinzani kwa kupanga maandamano hayo AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Wito wa viongozi hao umekuja wakati huu maofisa wa polisi wakikabiliana na waandamanaji waliokuwa wamekarishwa na kuchaguliwa tena kwa rais Azali Assoumani.

Kwa mujibu wa maofisa wa tume ya uchaguzi, Assoumani aliibuka mshindi wa uchaguzi huo baada ya kupata asilimia 62.97 ya kura zote zilizopigwa siku ya Jumapili.

Licha ya tangazo hilo la tume ya uchaguzi, wapinzani watano walioshiriki uchaguzi huo wamesema kuwa kulikwepo na udaganyifu na wizi wa kura.

 

Kwa mujibu wa wagombea wa upinzani, uchaguzi huo ulikumbwa na udaganyifu
Kwa mujibu wa wagombea wa upinzani, uchaguzi huo ulikumbwa na udaganyifu © AFP / OLYMPIA DE MAISMONT

Kabla ya tangazo hilo la upinzani, polisi walikuwa wamewatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi walipokuwa wakijaribu kufunga barabara kwenye jiji kuu.

Msemaji wa serikali Houmed Msaidie, ametuhumu upinzani kwa kupanga maandamano hayo.

Matokeo rasimi yaliotolewa siku ya Jumanne yalionyesha kuwa Assoumani, kiongozi wa zamani wa mapinduzi ambaye baadae alikuwa rais wa kiraia, aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa duru ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.