Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Comoro: Makabiliano yazuka Moroni baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais

Wanajeshi wametumwa Moroni, baada ya makabiliano kuzuka Jumatano Januari 17 asubuhi huko Comoro. Maandamano yaliripotiwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu saa chache baada yakutangazwa kwa matokeo ya muda ya uchaguzi wa urais siku ya Jumanne kwa kuchaguliwa tena kwa Rais Azali Assoumani. Wakati waangalizi wa kimataifa walibaini kwamba uchaguzi huo ulikuwa huru na wa uwazi kwa ujumla, upinzani na sehemu ya watu walianza kueleza kutokubaliana kwao.

Wanajeshi wametumwa katika mitaa ya Moroni, karibu na soko la Volo Volo, Jumatano Januari 17.
Wanajeshi wametumwa katika mitaa ya Moroni, karibu na soko la Volo Volo, Jumatano Januari 17. © David Baché / RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Kutoka kwa mandishi wetu maalum kwa Moroni,

Jumatano asubuhi, kuanzia saa nne asubuhi kwa saa za Comoro (sawa na saa tatu saa za Afrika ya Kati), maandamano yaliripotiwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Comoro.

Askari wanmekuwa wakirusha mawe karibu na nyumba na kuwaambia watu waende nyumbani. "Raia hawana furaha. Kwa sababu ya uchaguzi, ambao umevurugwa, ni jambo la kuchekesha,” amesema mpita njia karibu na soko la Volo Volo, akikatizwa na gari lililojaa polisi likiendeshwa kwa mwendo wa kasi na kupiga honi.

Wakati waangalizi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) na Umoja wa Afrika (AU) wakibaini kwamba uchaguzi huo  ulikuwa huru na wa uwazi, upinzani unapinga matokeo hayo na kukemea mchakato wa uchaguzi unoumpa ushindi wa rais anayemaliza muda wake Azali Assoumani, ambaye alipata 62.97. % ya kura. Kutowiana kwa takwimu za ushiriki zilizotangazwa Jumanne kumeimarisha shutuma za upinzani za udanganyifu mkubwa uligubika uchaguzi huo.

Hali tete na matukio katika sehemu mbalimbali

Saa chache baada ya kuanza kwa makabiliano hayo, hali bado ni tete lakini hali ya wasiwasi ya asubuhi imepungua karibu na soko kubwa la Volo Volo. Matukio, hata hivyo, yanaripotiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali katika mji mkuu - iwe katika wilaya ya Coulée, kwenye Uwanja wa Uhuru - au hata katika mji wa Ikoni. Hii ni kwa maandamano yanayozuka na kisha kupungua.

Wanajeshi, polisi na maafisa wa idara za usalama wametumwa kwa wingi na kuzunguka jiji. Mabomu ya machozi yalirushwa, waandamanaji waliweka vizuizi vya matawi au matairi katika maeneo mbalimbali, hasa kwenye barabara inayoelekea uwanja wa ndege.

Matairi yamejengwa kama kizuizi. "Kulikuwa na uchaguzi hapa Comoro, Rais Azali Assoumani ameibuna mshindi, na ndiyo maana tunaingia barabarani," anaeleza mmoja wa waandamanaji.

Hospitali Kuu ya Kitaifa inataka "kujilinda" kupokea watu wanaoweza kujeruhiwa

Mfanyikazi wa Hospitali Kuu ya Kitaifa, karibu na soko, anasema kuwa "katika mji mkuu, watu wengi wamekusanyika. "

Kwa sasa, vitendo hivyo vinaonekana kuwa vuguvugu la ghafla la wakaazi wenye hasira wanaoamini kuwa matokeo ya urais yaliyotangazwa yalichakachuliwa.

Tangu matokeo haya ya uchaguzi yatangazwe, hakuna hata mmoja kati ya wagombea watano wa upinzani aliyezungumza hadharani... Makada kutoka vyama vya upinzani walijitokeza kukemea takwimu hizo kwa nguvu zote, lakini bila kuitisha ghasia.

Kikihojiwa na RFI, chanzo cha serikali kimebaini kwamba upinzani hautaki kukubali kuwa umeshindwa na unaeleza kuwa kuna watu walikamatwa Jumatano asubuhi, bila kutaja idadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.