Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Comoro: Hali ya wasiwasi yatanda baada ya uchaguzi, uinzani walalamikia udanganyifu

Matukio kadhaa yameripotiwa siku ya Jumatatu katika visiwa vya Comoro vya Anjouan, ngome ya upinzani, na Mohéli, siku moja baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais katika visiwa vya Bahari ya Hindi. Rais anayemaliza muda wake Azali Assoumani anayepewa nafasi ya kushinda uchaguzi anashindana katika uchaguzi huo na wagombea wengine watano.

Kituo cha kupigia kura cha Moroni, Comoro, wapiga kura 338,000 wameitwa kupiga kura kuchagua magavana wao na hasa rais wao, Jumapili hii, Januari 14, 2024.
Kituo cha kupigia kura cha Moroni, Comoro, wapiga kura 338,000 wameitwa kupiga kura kuchagua magavana wao na hasa rais wao, Jumapili hii, Januari 14, 2024. © David Baché/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kucheleweshwa kwa zoezi la upigaji kura, kukosa vifa vya uchaguzi katika maeneo ambayo kijadi yanamkosoa mkuu wa nchi ambaye anashikilia nchi hiyo kwa mkono wa chuma, kuzuiwa kwa waangalizi katika zoezi la upigaji kura: upinzani ulilaani dosari nyingi siku ya Jumapili. Uchaguzi huu wa urais, ambao matokeo yake yatatangazwa wiki hii, na uchaguzi wa magavana wa visiwa vitatu vya Comoro, nchi yenye wakazi 870,000 (Grande Comore, Anjouan na Mohéli), umechafuliwa na "udanganyifu wa uchaguzi" lakini pia " ujazo wa kura katika masanduku ya kura kinyume cha sheria", upinzani umelaani.

Wakiwa katika mji mkuu wa Moroni, bado mvua inanyesha, kila mtu alionekana kurudi kwenye shughuli za kawaida, mvutano mkubwa ulitawala Anjouan, ambapo vijana walijitokeza wenyewe baada ya kutangazwa kwa ushindi wa kudhaniwa wa mgombea wa chama tawala. Gavana wake wa sasa, Anissi Chamsidine, aliyewasiliana kwa njia ya simu na shirika la habari la AFP, ameshutumu "ukosefu wa uwazi na usawa" na kutilia shaka "uadilifu wa mchakato wa uchaguzi".

Anaielezea "hali ya wasiwasi", maandamano ya moja kwa moja na "milipuko inayosikika" huko Mutsamudu, ngome ya mpinzani mkuu wa zamani wa mkuu wa nchi, rais wa zamani maarufu Ahmed Abdallah Sambi, anayezuiliwa jela kwa rushwa katika kesi iliyotajwa kutofuata haki. "Tuko katika makao makuu yetu huko Mutsamudu na tulipigwa gesi na polisi," anasema François Botsy wa chama cha Juwa. "Vijana walibaini, milipuko ilisikika, kutoka kwa polisi ili kutawanya umati wa waandamanaji," anaongeza Mahmoud Elrif, wa chama hicho.

Huko Mohéli, kisiwa kidogo chenye wapiga kura wapatao 25,000 pekee, hali pia ilisalia kuwa ya wasiwasi. Chama tawala "kinataka matokeo ya udanganyifu" na kutangaza ushindi wa mgombea wake wa ugavana katika duru ya kwanza, Abdoulanziz Hassanaly, mgombea wa upinzani kwenye nafasi hiyo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Meneja wake wa kampeni "amejeruhiwa na polisi wakati waandamanaji walipokuwa wakijaribu kwenda kwa tume ya uchaguzi," amesema. "Watu waliingia mitaani." "Jeshi lilisambazwa kila mahali Fomboni", mji mkuu, "wananchi walifunga barabara", anasema mkazi wa eneo hilo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye hakutaka jina lake litajwe. Lakini hakukuwa na "majeruhi wala watu kukamatwa", anaelezea Ibrahim Aballah, mkuu wa jeshi katika kisiwa hicho. "Waandamanaji walikuwa wakirusha mawe lakini hali sasa imedhibitiwa."

Takriban wapiga kura 340,000 waliitwa kupiga kura siku ya Jumapili. Kulingana na tume ya uchaguzi, ambayo ilikaribisha uchaguzi "wa amani na utulivu" siku ya Jumapili, kiwango cha ushiriki kilizidi 60%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.