Pata taarifa kuu

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika visiwa vya Comoro

Nairobi – Kura zinahesabiwa katika visiwa vya Comoro, baada ya wananchi kupiga kura hapo, kumchagua rais na wabunge. Rais Azali Assoumani, anatafuta muhula wa pili na anapambana na wagombea wengine watano, wanaokosoa namna zoezi la upigaji kura lilivyofanyika.

Rais wa Comoro, Azali Assoumani anawania kwa muhula wa nne
Rais wa Comoro, Azali Assoumani anawania kwa muhula wa nne TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu, ulisusiwa na baadhi ya wanasiasa wakuu wa upinzani kwa kile wanachodai uchaguzi huo, hauwezi kuwa huru na haki.

Rais wa sasa Azali Assoumani anakabiliwa na upinzani kutika kwa wapinzani watano wakati huu anapowania muhula wan ne.

Mouigny Baraka Saïd Silihi ni mmoja wa wagombea wa upinzani.

“Katika vitongoji vingi, jeshi lilikusanya matokeo na kuyapeleka kwenye kambi ya polisi.” alisema Mouigny Baraka Saïd Silihi

Uchaguzi huu, ulisusiwa na baadhi ya wanasiasa wakuu wa upinzani kwa kile wanachodai uchaguzi huo, hauwezi kuwa huru na haki.

Timu ya kampeni  ya Assoumani imekanusha madai hayo ya upinzani kwamba kulikuwepo na udaganyifu.

Matokeo ya awali yatatolewa ndani ya wiki moja, kwa mujibu wa baraza la uchaguzi Ceni.

Iwapo hakuna mgombea hata mmoja kati ya sita atapata zaidi ya 50% ya kura, wagombea wawili walio na kura nyingi zaidi wataelekea kwenye duru ya pili ya uchaguzi tarehe 25 Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.