Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Comoro: Kuidhinishwa kwa waangalizi na wawakilishi wa upinzani bado kunaleta tatizo

Nchini Comoro, wapiga kura 338,000 wanatarajiwa kupiga kura Jumapili hii Januari 14 kwa ajili ya kuwachagua magavana wao na rais wao.Wapinzani watano wanaochuana kwenye uchaguzi wa urais wakilalamikia kutopokea vibali kwa wakati na kushutumu Tume ya Uchaguzi kusababisa tatizo hilo. Tume ya Uchaguzi ilitangaza maelewano siku ya  Ijumaa, Januari 12, ikikubali kukwepa baadhi ya vifungu vya kisheria ili kuridhisha upinzani na kuruhusu wawakilishi wake kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

Wajumbe wa vituo vya kupigia kura kutoka wilaya zote za Comoro wakila kiapo kabla ya uchaguzi wa urais tarehe 14 Januari 2024.
Wajumbe wa vituo vya kupigia kura kutoka wilaya zote za Comoro wakila kiapo kabla ya uchaguzi wa urais tarehe 14 Januari 2024. © David Baché/RFI
Matangazo ya kibiashara

Matokeo yake, kambi ya rais nayo inaapinga kwa upande wake. Uongozi wa kampeni ya Azali Assoumani "unazingatia kwamba wagombea wanaoanzisha ombi hili ambalo halijawahi kushuhudiwa watawajibika" kwa matokeo ya uwezekano wa uamuzi huu unaoelezewa kuwa "kinyume cha sheria" na ambao "utahatarisha uendeshaji mzuri wa uchaguzi. » Kwa upande wake, upinzani unaendelea kuhofia “mapinduzi ya uchaguzi. "

Waangalizi wa kitaifa na kimataifa wanatakiwa kufuatilia upigaji kura. Misheni za kimataifa zimepata vibali vyao, lakini sio mashirika ya kiraia ya Comoro, ambayo bado yanaelezea Jumamosi jioni hii kwamba wanajaribu kupata hadi dakika ya mwisho kutoka CENI na hawafichi wasiwasi wao juu ya hatari za udanganyifu. Kwa upande wake, Tume ya Uchaguzi inatambua ucheleweshaji, lakini inahakikisha kwamba "wengine tayari wamekusanya beji zao".

Azali Assoumani, aliye madarakani tangu 2016, anatafuta muhula mpya. Wakimkabili, wagombea watano wanaotia mbele kupishana madarakani. Sehemu ya upinzani inataka kususia uchaguzi huo. Upinzani unaonyesha hofu nyingi kuhusu uwazi na uaminifu wa uchaguzi. Mabadiliko haya ya hivi punde na mvutano huu wa mwisho kati ya kambi ya urais na wagombea wa upinzani unashuhudia zaidi hali ya kutoaminiana na mvutano ambapo wananchi wa Comoro wanaitwa kupiga kura Jumapili hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.