Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Comoro: Chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi, kampeni zaendelea kwa kasi kubwa

Januari 14, wananchi wa Comoro watatumia haki yao ya kupiga kura kumchagua rais wao mpya ambaye ataiongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo. Wagombea sita, akiwemo Rais wa sasa Azali Assoumani, wako katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huu muhimu. Lakini kampeni za uchaguzi, ambazo zilianza Desemba 17, 2023, zilianza vibaya.

Mkutano wa chama cha Orange mjini Moroni, Comoro, Novemba 5, 2023.
Mkutano wa chama cha Orange mjini Moroni, Comoro, Novemba 5, 2023. © Abdallah Mzemballah
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Morono, Abdallah Mzembaba

Kwa upande wa upinzani, msisitizo umewekwa katika kurejea kwa utaratibu wa kikatiba wa mwaka 2001, ambao ulitoa nafasi ya urais kwa zamu kila baada ya miaka minne kati ya visiwa mbalimbali. Kurejeshwa kwa utawala wa sheria pia ni jambo kuu lililotolewa.

Lengo lingine linalowahusu wagombea wote wa upinzani, ni mapambano dhidi ya gharama za maisha na ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana. Mapendekezo madhubuti yanatolewa, kama vile huduma ya dharura bila malipo katika hospitali za umma, kupunguzwa kwa ushuru wa forodha na hatua za kusuluhisha mzozo wa elimu, unaochochewa sasa na mgomo usiokoma tangu Novemba 17, 2023.

Kwa upande wa Rais anayemaliza muda wake Azali Assoumani, ambaye anawania muhula mwingine, pamoja na kutetea rekodi yake, ametangaza nia ya kuendeleza miradi ya sasa, hasa katika nyanja ya miundombinu ya barabara, bahari na hospitali. Vipaumbele vingine vilivyojadiliwa ni pamoja na nishati mbadala na kupanua wigo wa kodi katika sekta ya uchumi. Lakini Azali Assoumani anasema utulivu wa kisiasa, umoja wa kitaifa na amani ndio maneno muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.