Pata taarifa kuu
UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais Comoro: Changamoto na ahadi za wagombea

Chaguzi mbili zitafanyika ndani ya wiki moja tu, Januari 14, huko Comoro. Uchaguzi unaotarajiwa zaidi ni uchaguzi wa urais, ambapo rais anayemaliza muda wake Azali Assoumani anatafuta muhula mwingine dhidi ya wagombea watano wa upinzani. Wacomori pia watawachagua magavana wao wapya. Ni changamoto gani kuu katika uchaguzi wa urais? Je, wagombea wanakusudia kujibu vipi? Je, uchaguzi unaonekana wa kuaminika?

Kutoka kushoto kwenda kulia: Bourhane Hamidou, Daoudou Abdallah Mohammed, Mouigni Baraka Saïd Soilihi, Aboudou Soefo, Salim Issa Abdillah na Azali Assoumani.
Kutoka kushoto kwenda kulia: Bourhane Hamidou, Daoudou Abdallah Mohammed, Mouigni Baraka Saïd Soilihi, Aboudou Soefo, Salim Issa Abdillah na Azali Assoumani. © Montage RFI - RFI/Abdallah Mzembaba
Matangazo ya kibiashara

Azali Assoumani anatafuta muhula mwingine. Ikiwa atachaguliwa tena, rais anayeondoka anatamani kuendeleza kazi iliyoanzishwa tangu mwaka 2016 na utekelezaji wa mpango wake "Plan Comoro émergent". Vipaumbele anaweka mbele: “Amani, usalama na demokrasia. " Ili kuvutia wawekezaji wa kigeni, Azali Assoumani anatetea "haki sawa": kamati ya kupambana na ufisadi iliyoundwa na sheria iliyopitishwa mwezi Septemba mwaka uliyopita inapaswa kutumiwa na Mahakama ya Juu. Rais anayemaliza muda wake pia anaahidi kuunda taasisi za kiufundi ili kuimarisha mafunzo ya vijana ili, kwa mara nyingine, kuvutia wajasiriamali lakini pia kuwazuia wahamiaji haramu wenye nia ya kuondoka nchi hiyo kuelekea Ulaya. Kwa upande wa afya, rais anayemaliza muda wake anapanga kuweka bima ya afya ya jumla.

Azali Assoumani ambaye alichaguliwa mwaka wa 2016, kisha akachaguliwa tena mwaka wa 2019 wakati wa uchaguzi wa mapema wa urais kufuatia marekebisho ya katiba, anaweza, ikiwa ataibuka mshindi tena, kusalia madarakani hadi mwaka 2029. Kama ukumbusho, Afisa huyu wa jeshi mwenye cheo cha Kanali aliongoza nchi hii baada ya mapinduzi ya mwaka 1999, kabla ya kuchaguliwa kidemokrasia mwaka 2002. Mwishoni mwa muhula wake mwaka 2006, hakutaka kubaki madarakani. Azali Assoumani mwenyewe pia anakumbusha kwamba tangu mwaka 2002, "nchi imepitia njia tano mbadala za kisiasa za amani".

Ugeuzaji maalum

Katiba ya Comoro inatoa nafasi ya urais wa kupokezana kati ya visiwa vitatu vinavyounda nchi hiyo - Grande Comore, Mohéli na Anjouan; na kisiwa cha nne ambacho ni Mayotte, kilichagua kuwa sehemu ya Ufaransa, mkoloni wake wa zamani. Lakini marekebisho ya katiba ya mwaka 2018 yanaidhinisha mihula miwili mfululizo ya miaka mitano kwenye nafasi ya urais, ikilinganishwa na muhula mmoja tu hapo awali. Hiki ndicho kinachomruhusu Azali Assoumani kugombea tena Januari 14. Na pia ni moja ya masualama kuu yanayojirudia katika programu za wagombea wa upinzani.

Bila kutilia shaka kanuni yenyewe ya urais wa kupokezana, baadhi wanashutumu kipengele kilichowekwa maalum cha kuongeza muda wa mamlaka ya Azali Assoumani na kuomba kurejea katika muhula mmoja wa miaka mitano, kama vile Mouigni Baraka Saïd Soilihi, wa chama cha Rassemblement démocratique des Comores pour l'égalité na Daoudou Abdallah Mohamed, kutoka chama cha Orange.

Kwa ajili hiyo, wagombea mbalimbali wa upinzani wanapendekeza kurekebisha Katiba au kupitisha mpya. Bourhane Hamidou, wa chama cha WONEHA, anataka kusimamishwa kwa maandishi ya kimsingi ambayo kwa sasa ni "kipaumbele chake cha kwanza".

Gharama ya maisha na elimu

Lakini wapiga kura, na kwa hivyo wagombea, pia wana wasiwasi zaidi na wa kila siku. Dhidi ya gharama kubwa ya maisha na mfumuko wa bei, Aboudou Soefo anapendekeza, kwa mfano, kupunguza ushuru wa forodha na kupambana dhidi ya uvumi wa wafanyabiashara. Mgombea wa chama cha Tsasi pia anataka "kufanyia kazi kwa haraka bima ya afya ya jumla" ili kupunguza gharama za afya kwa kaya. Daoudou Abdallah Mohamed anapendekeza kukabiliana na mfumuko wa bei kwa kurekebisha mfumo wa kodi, na kuongeza ajira kwa vijana. Salim Issa Abdillah, daktari na mgombea anapeperusha bendera ya chama cha Juwa, anaahidi kutokuepo kwa malipo kwa wagonjwa mahututi na kupunguzwa kwa ushuru wa forodha "kwa maisha yanayokubalika ya kila siku". Mouigni Baraka Saïd Soilihi, kwa upande wake, anakusudia kupunguza mtindo wa maisha wa serikali - mshahara wa rais, safari rasmi - kuelekeza ufadhili wa afya au elimu.

Wakati walimu wa umma walimaliza mgomo wa mwezi mmoja na nusu mnamo Januari 4 kwa ajili ya mishahara yao, wagombea hao karibu wote wanahutubia sekta ya elimu. Bourhane Hamidou anahakikisha kwamba hiki ni kingine cha vipaumbele vyake, Daoudou Abdallah Mohamed anaahidi kufanya kazi na washirika wa kijamii, Aboudou Soefo ana nia ya "kuweka demokrasia" elimu ambayo anachukia kwa sasa inapungua kwa umma "kwa faida binafsi".

Haki za binadamu na uaminifu wa kura

Wagombea wa upinzani hatimaye wanaelezea wasiwasi wao kuhusu uwazi wa kura hiyo. Daoudou Abdallah Mohamed anataka polisi kukaa mbali na mchakato huo na kutilia shaka uhuru wa mwenyekiti wa CENI (Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi). Bourhane Hamidou, kupitia msemaji wake, anakumbusha kwamba masharti ya kuitisha baraza la uchaguzi hayakuzingatia sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.