Pata taarifa kuu

Mauritania: Waswasi watanda kwa wanunuzi kufuatia ongezeko la ushuru wa forodha

Kwa siku kadhaa, malori kutoka Morocco yamekuwa yakirundikana kwenye kituo cha mpaka cha Guerguerat, kaskazini mwa Mauritania. Haya ni matokeo ya ongezeko la ushuru wa forodha knchini Mauritania kwa mboga zinazotoka nje ya nchi. Serikali ya Mauritania bado haijawasiliana rasmi kuhusu ongezeko hili.

Sokoni huko Nouakchott, Mauritania.
Sokoni huko Nouakchott, Mauritania. Xavier ROSSI/Getty
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Nouakchott, Léa Breuil

Shirika linalotetea na kulinda wanunuzi nchini Mauritania (FMPC) linaonya juu ya hatari za hatua hiyo ya serikali juu ya uwezo wa kununua kwa wanunuzi nchini Mauritania.

Katika soko hili la Morocco huko Nouakchott, bei ya mboga imeongezeka katika siku za hivi karibuni, wanasema wanunuzi kadhaa kama Zeinaba.

"Pilipili kwa ouguiya (fedha za Mauritani)1,000, sijawahi kusikia hivyo!" Kawaida tumekuwa tukiinunua kwa 500 au 600, hapi ni kiwango cha juu," anabainisha.

Kwa Ami, mfanyabiashara wa jumla ambaye anatoka Morocco, ongezeko hili ni tokeo la moja kwa moja la ongezeko la hivi karibuni la ushuru wa forodha kwa mboga zinazotoka nje ya nchi. Kulingana na baadhi ya wachukuzi hawa wa Morocco, ushuru wa forodha umeongezeka maradufu katika kituo cha mpaka cha Guerguerat.

"Ushuru wa shehena ya lori moja kwa sasa ni milioni 1, sawa na ouguiya ya zamani 500,000. Yote haya yanakuwa mzigo mkubwa kwa wanunuzi. Baadhi ya malori ambayo yanakataa kulipa ushuru yanasalia kuzuiliwa Guerguerat na bidhaa ziko hatarini kupotea,” anaeleza.

"Mauritania inazalisha 10% tu ya mahitaji yake ya mboga"

Serikali ya Mauritania bado haijataka kuwasiliana rasmi kuhusu ongezeko hili la ghafla lakini, wiki hii, Waziri wa Uchumi, Abdessalam Ould Mohamed, alifafanua juu ya suala hili kwamba ilikuwa muhimu mara kwa mara kulinda uzalishaji wa ndani.

“Tuna haki ya kulinda uzalishaji wetu kwa msimu kunapokuwa na ushindani mkubwa na hatari ya hasara. Kwa mara nyingine tena tunaingia katika uzalishaji wa mazao ya bustani, lazima tuendelee kusaidia wajasiriamali wetu vijana,” anasema Waziri Abdessalem Ould Mohamed.

Hoja hii kutoka kwa Waziri wa Uchumi haikubaliki, kulingana na Awa Mohamed, mjumbe wa shirika linalotetea na kulinda wanunuzi nchini Mauritania.

"Mauritania inazalisha tu 10% ya mahitaji yake ya mboga. Nadhani kisingizio hiki hakifanyi kazi kiuchumi. Tunapoangalia umaskini mkubwa sana tunaiomba serikali ipunguze ushuru wa forodha na kodi kwa ujumla! ", anasema sAwa Mohamed kutoka FMPC.

Ongezeko la ushuru wa forodha linaweza kudumu katika msimu wote wa mavuno. Miezi michache kabla ya Ramadhani, shirika linalotetea na kulinda wanunuzi nchini Mauritania linatoa wito kwa serikali kutafuta masuluhisho ya haraka ili kupunguza uwezo wa ununuzi wa wanunuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.