Pata taarifa kuu

Rais wa zamani wa Mauritania ahukumiwa kifungo cha miaka 5

Mahakama ya Nouakchott siku ya Jumatatu imemhukumu rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kifungo cha miaka mitano jela, akishtakiwa tangu mwezi wa Januari 2023 kwa kutumia vibaya mamlaka yake ili kujikusanyia mali nyingi.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz.
Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz. © AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Bw. Aziz amekuwa akijibu tangu Januari 25 akiwa na watu wengine kumi, ikiwa ni pamoja na Mawaziri Wakuu wawili wa zamani, mawaziri wa zamani na wafanyabiashara, mashitaka ya "utajiri haramu", "matumizi mabaya ya kazi", "ushawishi wa biashara" au "ufujaji fedha". Mahakama ilimshtaki kwa kujitajirisha kinyume cha sheria na utakatishaji fedha.

Mahakama iliamuru kutaifishwa kwa mali iliyopatikana kupitia vitendo hivi, na ikatangaza kunyang'anywa kwa Bw. Aziz haki zake za kiraia. Mohamed Ould Abdel Aziz alikaribisha hukumu hiyo bila kukurupuka.

Bw. Aziz, mwenye umri wa miaka 66, anakuwa mmoja wa wakuu wa nchi adimu waliopatikana na hatia ya kujitajirisha kinyume cha sheria katika utumiaji wa madaraka. Wenzake wanaohukumiwa na mahakama ya kitaifa au kimataifa ni hasa kwa uhalifu wa kumwaga damu, kama vile, kwingineko Afrika Magharibi, dikteta wa zamani wa Guinea Moussa Dadis Camara, aliyeshtakiwa tangu mwezi wa Septemba 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.