Pata taarifa kuu
SHERIA-HAKI

Mauritania: Rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz kufungwa miaka 20 jela

Mwendesha mashtaka ameomba kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kutwaliwa mali yake dhidi ya rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz. Akishtakiwa kwa kujitajirisha kwa njia haramu, matumizi mabaya ya mamlaka na utakatishaji fedha, Mohamed Ould Abdel Aziz alikuwa amejilimbikizia mali na mtaji wa euro milioni 67 wakati aliposhtakiwa mnamo Machi 2021.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz mjini Nouakchott tarehe 1 Agosti 2019.
Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz mjini Nouakchott tarehe 1 Agosti 2019. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Nouakchott, Léa Breuil

Kesi ya siku ya Jumanne iliyochukua karibu saa tatu ambapo mwendesha mashtaka Ahmed Ould Moustapha alitangaza kwamba "vielelezo vyote vilivyo mikononi mwa ofisi yake vinathibitisha 

 kuwa rais huyo wa zamani alifanya uhalifu". Kwa hiyo aliomba kifungo cha miaka 20 jela dhidi ya rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye anashitakiwa, miongoni mwa mambo mengine, kwa kujitajirisha kinyume cha sheria. Pia aliomba kunyang'anywa mali yake.

"Anastahili hii kwa sababu uhalifu ni mbaya sana na ulio wazi. Ushahidi ni mwingi. Ushahidi wote upo ili apate hukumu ya juu zaidi. Rais wa Jamhuri anayetumia taratibu kujitajirisha na ambaye anatumia mali ya shirika kwa manufaa ya umma kutengeneza nyumba yake na kununua majengo ni hatia,” anasema wakili Vadili Raiss, Wakili Mkuu wa Serikali.

Lakini shtaka hili linapingwa vikali na mawakili wa utetezi wa mkuu wa zamani wa nchi. "Katika kesi hii, kuna vikao tu na hatuamini kuwa vikao vinaweza kufichua uhalifu wa kiuchumi. Hii ni kesi ambayo imewekwa pamoja tangu mwanzo kwa hivyo tunatarajia chochote lakini tunaamini kwamba tumejikita vya kutosha kisheria ili kufuta maombi yote ambayo yanaunda msingi wa matakwa ya upande wa mashtaka," amebainisha wakili Taleb Kyar.

Mwendesha mashtaka pia aliomba, pamoja na mambo mengine, kifungo cha miaka 10 jela dhidi ya mawaziri wakuu wawili na mawaziri wawili wa rais huyo wa zamani. Hatua inayofuata ya kesi: hoja za mwisho za upande wa utetezi kabla ya jaji kutoa uamuzi wake wa mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.