Pata taarifa kuu

Mauritania: Rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz alazwa hospitalini

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, akiwa kizuizini kwa muda wa miezi sita katika kesi ya madai ya ufisadi, analazwa tangu Jumatano jioni wiki hii katika hospitali ya kijeshi huko Nouakchott kwa huduma ya matibabu ya dharura.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, hapa ilikuwa Nouakchott Agosti 1, 2019, anafungwa kwa miezi sita sasa.
Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, hapa ilikuwa Nouakchott Agosti 1, 2019, anafungwa kwa miezi sita sasa. Seyllou / afp
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na watu wa familia yake waliomtembelea, hali ya rais huyo wa zamani wa Mauritania inatia wasiwasi. Mawakili wake pia walimtembelea. Walitarajia kuwa rais huyo wa zamani alitakiwa kulazwa hospitalini kutokana na hali ya afya ya mteja wao kuzorota kwa miezi kadhaa. Mwalimu Taleb Khiyar, mjumbe wa kundi la ulinzi la Mohamed Ould Abdel Aziz.

“Kwa muda wa miezi sita, tumeomba kwa wakati, kwa njia thabiti, kwa mamlaka husika, hasa mamlaka za mahakama, tupate haki ya kumtembelea ili kujua hali yake kwa sababu tulijua hilo litatokea wakati fulani, kwani angepatwa na matatizo ya kiafya kwa sababu zifuatazo. Kwanza, inanyimwa haki ya kupata mwanga wa jua. Huwezi kufikiria kwamba mtu anaweza kuishi miezi sita katika chumb kidogo bila kuona jua, na kwamba anakabiliwa na hatari za kuzorota kwa afya. Hii haiwezekani kulingana na mtazamo wa kisayansi. Tunaendelea kutoa wito wa kuachiliwa kwake hivi karibuni au watafute njia ya kumpeleka katika nchi ambayo anaweza kutibiwa kwani, kwa kweli, hali yake ni mbaya sana na tuna hofu kwamba itazidi kuwa mbaya. "

Rais huyo wa zamani alishtakiwa mwezi Machi kwa rushwa, utakatishaji fedha, kujitajirisha kinyume cha sheria, ubadhirifu wa mali ya umma, kutoa manufaa yasiyostahili na kuzuia mahakama kufanya kazi yake. Mashtaka yaliyokanushwa na rais huyo wa zamani aliyetawala nchi hiyo kati ya mwaka 2008 na 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.