Pata taarifa kuu
MAURITANIA

Mauritania: Mauritania kuadhimisha miaka 60 ya uhuru

Jumamosi hii Novemba 28, Mauritania inaadhimisha miaka 60 ya uhuru wake, wakati wengi miongoni mwa wananchi wa taifa hilo wanaendelea kujiuliza iwapo wamepiga hatua kwa yale yaliyoafikiwa baada ya uhuru huo.

Bendera ya Mauritania.
Bendera ya Mauritania.
Matangazo ya kibiashara

Mengi yalitarajiwa kufikiwa baada ya uhuru huo mnano mwaka 1960, lakini kufikia sasa hayajakamilika, hususan suala la umoja na mshikamano wa kijamii. Suala ambalo lilizua gumzo wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais ambapo wengi walimuomba rais Mohamed Ould Ghazouani, kuchukua hatua mpya.

 

Mauritania ni nchi ya mwisho barani Afrika katika nchi zilizotawaliwa na Ufaransa kupata uhuru mnamo mwaka 1960. Nchini Mauritania, ujenzi wa taifa hilo changa ulikuwa ngumu sana.

 

Alipoulizwa juu ya kile anachokumbuka siku Mauritania ilipopata uhuru, mwanadiplomasia wa zamani na waziri wa zamani Taki Ould Sidi, ambaye siku hiyo alikuwa na umri wa miaka 18 anasema Mauritani imepiga hatua kubwa katika nyajna mbalimbali, kwani kabla ya uhuru nchi hiyo ilikuwa kama msitu.

 

Anasema "kikao cha kwanza cha mawaziri baada ya Mauritania kupata uhuru, kilifanyika katika hema! "

 

Mwasisi wa uhuru Moktar Ould Daddah pia anakumbuka changamoto Mauritani iliyopitia katika siku za mwanzo za baada ya uhuru. "Uhuru ulitangazwa katika jengo ambalo lilikuwa bado halijakamilika, na katika jengo hilo ndipo walipokelewa wageni wote wa nchi za kigeni walioalikwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo.

 

Wengi nchini Mauritania wanaamini kwamba nchi yao imepiga hatua katika nyanja mbalimbali, lakini kuna baadhi ya masuala muhimu ambayo hayakamilika, suala la umoja na mshikamano wa kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.