Pata taarifa kuu
MAURITANIA

Makumi ya wahamiaji watoweka Mauritania

Karibu wahamiaji 40, ikiwa ni pamoja na watoto watatu, wanaripotiwa kutoweka na kudhaniwa wamekufa maji baada ya injini ya boti lao kupatwa na tatizo walipokuwa wakijaribu kutua katika Visiwa vya Canary, Uhispania, wakitokea Sahara Magharibi, Shirika la Kimataiafa la Uhamiaji (IOM) limeripoti.

Wahamiaji wengi wamefariki dunia katika safari kama hizi, wakijaribu kuingia Ulaya.
Wahamiaji wengi wamefariki dunia katika safari kama hizi, wakijaribu kuingia Ulaya. REUTERS/Umit Bektas/File Photo
Matangazo ya kibiashara

IOM likinukuu shuhuda za manusura saba waliookolewa na maafisa wa kikosi cha ulinzi wa pwani ya Mauritania, limesema kwamba boti hilo iliyokuwa imebeba watu 54 kwenye iliondoka katika mji wa Laayoune mwanzoni mwa mwezi huu.

Wahamiaji wengi wamefariki dunia katika safari kama hizi, wakijaribu kuingia Ulaya, baada ya kuzitoroka nchi zao kutokana na sababu mbalimbali.

Wengi wanaona kuwa Ulaya ndio wanaweza kupata maisha mazuri ikilinganishwa na mazingira wanayoishi katika nchi zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.