Pata taarifa kuu
WAHAMIAJI

Wahamiaji zaidi ya 700 waokolewa katika Bahari ya Mediterania

Zaidi ya wahamiaji 700 wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediterania kwa boti kuingia Ulaya waliokolewa mwishoni mwa wiki, hasa Malta na Libya, shirika lisilo la kiserikali, SOS Méditerranée, limetangaza.

Wahamiaji wanasubiri kuokolewa na waokoaji kutoka mashirika ya SOS Méditerranée na Madaktari Wasio na Mipaka, Mei 24, 2016, katika pwani ya Libya.
Wahamiaji wanasubiri kuokolewa na waokoaji kutoka mashirika ya SOS Méditerranée na Madaktari Wasio na Mipaka, Mei 24, 2016, katika pwani ya Libya. GABRIEL BOUYS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumamosi, zoezi sita za uokoaji zilifanyika katika maji ya kimataifa, na zoezi la mwsho lilifanyika Jumapili alasiri, na watu 106 waliokolewa katika pwani ya Malta, limesema shirika hilo lisilo la kiserikali la SOS Méditerranée, lenye makao yake makuu Marseille.

"Mtoto wa umri wa miezi mitatu ni miongoni mwa watu waliookolewa jana Jumapili," SOS Méditerranée imeongeza.

Watu 400 waliokolewa siku ya Jumamosi katikati ya bahari ya Mediterania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.