Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Rais wa zamani wa Mauritania Aziz, aliyeshtakiwa kwa ufisadi, aachiliwa

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz ambaye alikuwa akizuiliwa jela kwa kashfa mbalimbali yuko huru tngu Jumatano usiku baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa uamuzi wa mahakama, akisubiri kusikilizwa kwa tuhuma za ufisadi, amebainisha mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz. (Picha ya iliyopigwa mwaka wa 2018).
Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz. (Picha ya iliyopigwa mwaka wa 2018). © AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Karibu saa sita usiku Alhamisi, maafisa wa polisi walianza kuondoa vizuizi karibu na nyumba yake katika mji mkuu wa Nouakchott, na maafisa waliopewa kazi na mahakama ya kumfuatilia walianza kuondoka. Bw Aziz, ambaye aliongoza Mauritania kuanzia mwaka wa 2008 hadi 2019 na ana umri wa miaka 65, alitoka nje ya nyumba yake na kuwapungia mkono watu wachache waliokuja kusherehekea uhuru wake wa kutembea tena.

"Uhakiki wake wa mahakama ulimalizika Jumatano hii usiku wa manane na, kama inavyotakiwa na sheria, yuko huru kutembea, Lakini haimaanishi kuwa kesi yake imefungwa," jaji mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia sjhirika la habari la AFP.

Kiongozi huyo wa zamani wa Mauritania alishtakiwa mwezi wa Machi 2021 pamoja na viongozi kadhaa waandamizi kwa tuhuma za vitendo vya rushwa, utakatishaji fedha, utajiri haramu, ubadhirifu wa mali ya umma, kutoa faida isivyostahili na kuzuia kazi ya mahakama.

Rais huyo wa zamani na washtakiwa wengine, wakiwemo wakwe zake, mawaziri wakuu wawili wa zamani, mawaziri kadhaa wa zamani na wafanyabiashara kadhaa, sasa wanarudishwa mahakamani. Hakuna tarehe iliyowekwa kwa kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.