Pata taarifa kuu
NIGER-HAKI

Mauritania: Aliyekuwa rais wa Mauritania Abdel Aziz kuachiliwa kwa sababu za kiafya

Mahakama ya Mauritania ilikubali Ijumaa kwa sababu za kiafya kumwachilia chini ya uangalizi wa mahakama rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz, anayezuiliwa kwa miezi kadhaa katika kesi ya madai ya ufisadi, imetangaza wizara ya Sheria.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz na watu kadhaa wa familia yake walichunguzwa hasa kuhusiana na tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma.
Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz na watu kadhaa wa familia yake walichunguzwa hasa kuhusiana na tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma. LUDOVIC MARIN / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Ould Abdel Aziz, 65, alilazwa hospitalini mwishoni mwa mwezi Desemba kwa uangalizi wa haraka baada ya kuugua, kulingana na mawakili wake. Januari 1, alifanyiwa upasuaji wa moyo uliolenga kupanua mishipa na kukuza mzunguko wa damu. Zoezi ambalo lilienda vizuri, kulingana na duru kutoka hospitali.

Madaktari wanaomfuatilia wamesema, katika ripoti, "anatakiwa kuwa katika hali isio yawasiwasi na shinikizo la kisaikolojia," wizara ya sheria imesema katika taarifa.

Kwa hivyo, upande wa mashtaka uliomba aachiliwe na majaji waliosimamia uchunguzi walikubali kwamba awekwe chini ya uangalizi wa mahakama na kuhudumiwa kimatibabu nyumbani kwake, wizara imebainii.

Aziz, ambaye aliongoza Mauritania kutoka mwaka 2008 hadi mwaka 2019, alifungwa katika mazingira mazuri, majibu "ya haraka na ya ufanisi" kutoka kwa huduma za Serikali kwa kuzorota kwa afya yake na "kupata huduma ya juu ya matibabu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.