Pata taarifa kuu

Mauritania: Serikali yahakikishia umma kuhusu hali ya afya ya Mohamed Ould Abdel Aziz

Nchini Mauritania, rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz yuko hospitalini kwa usiku wake wa tatu. Baada ya kulazwa siku mbili katika hospitali ya kijeshi ya Nouakchott, aliingizwa hospitali usiku wa manane, kwa saa za nchini Tunisia katika kituo cha magonjwa ya moyo cha Nouakchott ambapo wataalamu watatu walimhudumia kwa vipimo.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz.
Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz. © AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Hali ya afya ya rais huyo wa zamani inatia moyo, kulingana na taarifa iliyotolewa Ijumaa alasiri kutoka Wizara ya Sheria. Kwa hiyo hakuna hofu na ni madaktari tu wanaohusika ndio wenye uwezo wa kutoa taarifa.

Lakini tangazo hili la serikali ya Mauritania saa 72 baada ya kulazwa hospitalini kwa Mohamed Ould Abdel Aziz, haijaridhisha familia na mawakili wa rais huyo wa zamani. Wanasisitiza na wanaendelea kudai kuwa Mohamed Ould Abdel Aziz ana matatizo makubwa ya moyo. Shinikizo lake la damu huzidi kupanda, kulingana na mmoja wa binti zake.

Mohamed Ould Abdel Aziz anashtakiwa kwa ufisadi, utakatishaji fedha na kujitajirisha kinyume cha sheria. Tuhuma ambazo alikanusha kila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.