Pata taarifa kuu

Miili 16 inayodhaniwa kuwa ya wahamiaji imepatikana pwani ya Mauritania

Mamlaka nchini Mauritania imethibitisha kupatikana kwa miili 16 kaskazini mwa pwani ya taifa hilo, miili inayodhaniwa kuwa ya wahamiaji.

Wahamiaji wengi hutumia boti za mbao wakiwa na nia ya kuingia barani Ulaya wakitokea Afrika
Wahamiaji wengi hutumia boti za mbao wakiwa na nia ya kuingia barani Ulaya wakitokea Afrika AP - Felipe Dana
Matangazo ya kibiashara

Miili hiyo ambayo imepatikana katika visiwa vya Lagouera imegunduliwa ikiwa imepita wiki moja tangu kupatikana kwa miili ingine 13 kwenye boti kwenye eneo hilo karibu na mji wa Nouadhibou.

Kwa mujibu wa mamlaka, huenda, watu hao walifariki baada ya boti lao kugonga jiwe.

Kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu wanaotokea katika nchi jirani ya Senegal wakiwa na lengo na kufika katika visiwa vya Canary nchini Uhispania.

Tangu mwezi Januari, zaidi ya watu elfu 23 wamewasili katika visiwa hivyo kwa kutumia boti.

Vijana wengi kutoka bara Afrika wamekuwa wakitumia njia hatari kuingia nchini Uhispania
Vijana wengi kutoka bara Afrika wamekuwa wakitumia njia hatari kuingia nchini Uhispania © Europa Press via AP

Idadi kubwa ya raia kutoka nchi za bara Afrika wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa kutumia usafiri hatari wa majini wakitaka kuvuka kwenda Ulaya kutafuta maisha bora.

Suala hili limetajwa kusababishwa na ukosefu wa ajiri katika mataifa ya bara Afrika, wengi wa vijana wakiendelea kutoa wito kwa serikali zao kuwajengea nafasi za ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.