Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa watoa wito wa kuachiliwa kwa raia waliotekwa nyara nchini Cameroon

Umoja wa Mataifa umetoa wito Alhamisi "kuachiliwa haraka" kwa watu waliotekwa nyara wakati wa shambulio la hivi majuzi kwenye soko moja magharibi mwa Cameroon lililohusishwa na mamlaka na waasi wanaotaka kujitenga wanaozungumza Kiingereza.

Mgogoro kati ya waasi wanaotaka kujitenga wanaozungumza Kiingereza na Cameroon umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kutoroka makaazi yao, kulingana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia mizozo, ICG.
Mgogoro kati ya waasi wanaotaka kujitenga wanaozungumza Kiingereza na Cameroon umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kutoroka makaazi yao, kulingana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia mizozo, ICG. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tunasikitishwa na shambulio la Novemba 21 kwenye soko la Bamenyam magharibi mwa Cameroon, ambapo raia tisa waliuawa. Waliohusika lazima wawajibishwe," amesema msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, Seif Magango katika maoni yaliyotumwa kwa waandishi wa habari.

"Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wanaotaka kujitenga wenye silaha kutoka eneo linalozungumza Kiingereza la Kaskazini-Magharibi walivamia soko katika eneo linalozungumza Kifaransa la Bamboutos, wakifyatua risasi hovyo na kuchoma biashara. Pia waliwateka nyara angalau raia 10 na kupora mali," amesema.

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu inataka "kuachiliwa kwa haraka kwa watu wote waliotekwa nyara na kufanyike uchunguzi wa kina, usio na upendeleo na huru kuhusu mashambulizi yote dhidi ya raia kwa nia ya kuwawajibisha wahalifu."

Kijiji cha eneo la Magharibi ambako shambulio hilo lilifanyika kiko kwenye ukingo wa eneo la Kaskazini-Magharibi, linalokaliwa na watu wachache wanaozungumza Kiingereza wa Cameroon, nchi kubwa katika Afrika ya Kati hasa inayozungumza Kifaransa.

Tangu mwisho wa mwaka wa mwaka 2016, mzozo mbaya umehusisha makundi ya kupigania uhuru na vikosi vya usalama katika mikoa ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, huku kila upande ukishutumiwa mara kwa mara kwa uhalifu dhidi ya raia na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi haya hutokea mara kwa mara katika mikoa hiyo miwili au kwenye mipaka, huku waasi wakiwashutumu baadhi ya wanavijiji kwa kushirikiana na serikali.

"Mashambulizi dhidi ya raia hayakubaliki," Magango amesema, akiongeza kuwa hili ni shambulio la pili kubwa kufanywa na makundi yenye silaha mwezi huu.

Mnamo tarehe 6 Novemba, raia 25, wakiwemo wanawake na mtoto mmoja, waliuawa huko Egbekaw, katika eneo la Kusini-Magharibi, katika shambulio lililohusishwa na serikali ya Yaoundé dhidi ya watu wanaotaka kujitenga, ambao waliwaua baadhi ya wahanga na kuwachoma moto wengine.

Mzozo huo ulizuka mwishoni mwa mwaka 2016 baada ya Rais Paul Biya, ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa miaka 41, kukandamiza maandamano ya amani ya watu wanaozungumza Kiingereza katika mikoa hiyo miwili, ambao walihisi kutengwa na serikali kuu, katika koloni hili la zamani la Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.