Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Cameroon: Wanakijiji tisa wauawa na watu wanaozungumza Kiingereza wanaotaka kujitenga

Takriban wanakijiji tisa wameuawa siku ya Jumanne katika shambulio jipya magharibi mwa Cameroon linalohusishwa na mamlaka na waasi wanaozungumza Kiingereza wanaotaka kujitenga, ambao wamekuwa wakikabiliana na jeshi kwa miaka saba katika vita vilivyosababisha vifo vya raia.

Mgogoro kati ya waasi wanaotaka kujitenga wanaozungumza Kiingereza na Cameroon umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kutoroka makaazi yao, kulingana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia mizozo, ICG.
Mgogoro kati ya waasi wanaotaka kujitenga wanaozungumza Kiingereza na Cameroon umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kutoroka makaazi yao, kulingana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia mizozo, ICG. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Alfajiri, wavamizi hao walivamia soko katika kijiji cha Bamenyam, katika kaunti ya Bamboutos. "Watu tisa wameuawai," gavana wa Bamboutos, David Dibango, amesema kwenye redio ya serikali CRTV. "Nimehesabu vifo tisa," amethibitisha kwa njia ya simu kwa shirika la habari la AFP afisa wa jeshi ambaye aliomba kutotajwa jina na ambaye anahusisha "wanaotaka kujitenga" kwa mauaji hayo.

Kijiji hiki katika eneo la Magharibi kiko kwenye ukingo wa eneo la Kaskazini-Magharibi, linalokaliwa na watu wachache wanaozungumza Kiingereza nchini Cameroon, nchi kubwa ya Afrika ya Kati ambayo wengi wao huzungumza Kifaransa.

Tangu mwisho wa mwaka wa 2016, mzozo mbaya umehusisha makundi ya kupigania uhuru na vikosi vya usalama katika mikoa ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, huku kila upande ukishutumiwa mara kwa mara kwa uhalifu dhidi ya raia na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa. Mashambulizi haya hutokea mara kwa mara katika mikoa hiyo miwili au kwenye mipaka, huku waasi wakiwashutumu baadhi ya wanavijiji kwa kushirikiana na serikali.

Mnamo Novemba 6, raia 25, wakiwemo wanawake na mtoto mmoja, waliuawa huko Egbekaw, Kaskazini-Magharibi, katika shambulio lililofanywa na Yaoundé dhidi ya watu wanaotaka kujitenga, ambao waliwaua baadhi ya waathiriwana kuwachoma moto wengine. Kulingana na CRTV, mwanamke mmoja ni miongoni mwa waliouawa siku ya Jumanne huko Bamenyam. Maafisa polisi wawili waliojibu wamejeruhiwa, kulingana na vyombo vya habari vya serikali na maduka yalichomwa moto.

Mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 na wengine zaidi ya milioni moja kuyahama makazi yao, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia mizozo, ICG. Waasi, ambao wanajiita "Ambazonia" (kutoka kwa jina la "Ambazonia" ambalo uhuru wao walitangaza mwaka wa 2017), mara kwa mara huwashambulia raia ambao wanawatuhumu "kushirikiana" na Yaoundé.

Vikosi vya usalama pia vinashutumiwa mara kwa mara na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kwa "makosa", mauaji na mateso mengine ya raia ambayo wanashuku kuwa wanashirikiana na waasi.

Mwanzoni mwa mwezi wa Julai, shirika la kimataifa la haki za Binadamu la Amnesty International kwa mara nyingine tena ilishtushwa na "ukatili" unaowakumba raia, ikiorodhesha "mauaji kwa watu walio mikonoi mwa vyombo vya dola", "mauaji" dhidi  ya wanawake na watoto, "mateso" na "ubakaji", unaofanywa na waasi wanaotaka kujitenga, vivo hivyo kwa askari wa vikosi vya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.