Pata taarifa kuu

Cameroon: Maporomoko ya udongo yasababisha vifo vya karibia watu 23

Nairobi – Karibia watu 23 wamethibitishwa kufariki wakati wengine wakiwa hawajulikani waliko jijini Yaoundé nchini Cameroon baada ya maporomoko ya udongo kuharibu nyumba kadhaa katika eneo la Mbankolo.

Karibia watu 23 wameripotiwa kufariki katika maporomoko ya udongo
Karibia watu 23 wameripotiwa kufariki katika maporomoko ya udongo REUTERS - AMINDEH BLAISE ATABONG
Matangazo ya kibiashara

Maporomoko hayo ya udongo yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo tofauti ya mji huo siku ya Jumapili.

Shirika la habari la serikali kwa upande wake limeripoti vifo vya karibia watu 13 kutokana na janga hilo, idadi hiyo ikihofiwa kuongezeka.

Shughuli za uokozi zinaedelea katika eneo la tukio, idadi ya watu wasiojulikana waliko ikiwa haijawekwa wazi.

Idadi ya waliofariki inahofiwa kuongezeka
Idadi ya waliofariki inahofiwa kuongezeka REUTERS - AMINDEH BLAISE ATABONG

Mwezi Novemba mwaka jana, maporomoko ya udongo yalisababisha vifo vya karibia watu 14 waliokuwa wanahudhuria mazishi.

Tahadhari ya mafuriko ilitangazwa katika nchi jirani ya Nigeria siku ya Jumapili, mafuriko hayo yakihusishwa na maji ya yanayotoka katika bwawa la Mto Benue unaotiririka kutoka nchini Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.