Pata taarifa kuu

Cameroon imepokea shehena ya kwanza ya chanjo ya malaria

Nairobi – Umoja wa Mataifa umesema kuwa ongezeko linalokuja la chanjo ya malaria barani Afrika litakuwa mkombozi katika vita dhidi ya ugonjwa huo, baada ya shehena ya kwanza ya dozi kuwasili nchini Cameroon.

Hatua hii imetajwa kuwa mafanikio katika vita dhidi ya malaria
Hatua hii imetajwa kuwa mafanikio katika vita dhidi ya malaria © UNICEF
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa ya pamoja, Shirika la afya duniani WHO, UNICEF na kampuni ya chanjo ya Gavi, yamesema dozi hizi zaidi ya laki tatu, zinaashiria kuwa utoaji chanjo dhidi ya Malaria utaongezeka katika maeneo hatarishi zaidi barani humo.

Chanjo aina ya RTS,S ndiyo chanjo ya kwanza ya Malaria iliyopendekezwa na WHO, na inatolewa katika dozi nne, ya kwanza ikitolewa kwa watoto walio na umri wa miaka mitano, kukabiliana na kimelea cha plasmodium Falciparum ambacho ni hatari na kilichoenea zaidi barani Afrika.

Ndani ya wiki kadhaa zijazo, dozi zingine milioni 1 na laki 7 zitatolewa kwa nchi za Burkina Faso, Liberia, Niger na Sierra Leone.

Katika mwaka 2021, Afrika ilichangia takriban asilimia 95 ya matukio ya Malaria duniani na asilimia 96 ya vifo vinavyohusiana na ugonjwa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.