Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

DRC yatia saini makubaliano ya kupeleka wanajeshi wa SADC mashariki

Rais wa DRC, Félix-Antoine Tshisekedi aliongoza Ijumaa Novemba 17 hafla ya kusainiwa rasmi na upande wa Kongo mkataba wa kuweka hadhi ya kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambacho kitatumwa "katika siku zijazo" nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeandikwa kwenye ukurasa wa mdandao wa X wa Urais wa Jamhuri.

Rais wa DRC, Félix-Antoine Tshisekedi ameendelea kuishtumu Rwanda kuhatarisha usalama wa DRC, kupitia waasi wa M23.
Rais wa DRC, Félix-Antoine Tshisekedi ameendelea kuishtumu Rwanda kuhatarisha usalama wa DRC, kupitia waasi wa M23. © @RFIAfrique
Matangazo ya kibiashara

"Serikali ya Kongo kwa hivyo inajitolea kutoa kwa kikosi hiki ushiriki wa kidiplomasia unaohusishwa na aina hii ya uingiliaji kati. Hili pia linatimiza ahadi ya SADC ya kupeleka kikosi chake. Mkataba huu unafafanua madhumuni ya ujumbe wa jeshi la kikanda. Jeshi hili litatumwa kusaidia jeshi la DRC, FARDC, katika kupambana na kutokomeza kabisa M23 na makundi mengine yenye silaha ambayo yanaendelea kuvuruga amani na usalama nchini DRC,” mesema Waziri wa Mambo ya Nje, Christophe Lutundula.

Wakuu wa Nchi za SADC walikutana Novemba 4 mjini Luanda (Angola) katika mkutano usio wa kawaida kujadili hali ya Mashariki mwa DRC, tangu kuzuka upya kwa uasi wa M23 unaoungwa mkono na Rwanda, kulingana na serikali ya DRC, na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano huu, kulikuwa na mazungumzo maalum ya kutuma kikosi cha kikanda cha SADC kuchukua nafasi ya kile cha EAC.

Mnamo tarehe 10 Novemba, wakati wa Baraza la Mawaziri, Rais Félix-Antoine Tshisekedi aliwaalika Naibu Mawaziri Wakuu wa Mambo ya Nje na Ulinzi kufanya kila linalowezekana kufanikisha kutumwa kwa kikosi cha SADC nchini DRC.

Kwa hiyo mapendekezo yake yalifuatia mahitimisho ya mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi za SADC unaohusiana na kutumwa kwa Ujumbe wa SADC nchini DRC,  kulingana na na Radio Okapi inayorusha matangazo yake nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.