Pata taarifa kuu

DRC : Wakuu wa nchi za SADC wamejadili hali ya usalama mashariki ya nchi

Nairobi – Wakuu wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC walikutana kwa mfumo wa video kwa muda mfupi siku ya Jumanne, kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkutano huo unaelezwa ulitatizwa kwa sababu za kiufundi, na sasa wakuu hao wanajiandaa kukutana ana kwa ana siku ya Jumamosi, jijini Luanda nchini Angola
Mkutano huo unaelezwa ulitatizwa kwa sababu za kiufundi, na sasa wakuu hao wanajiandaa kukutana ana kwa ana siku ya Jumamosi, jijini Luanda nchini Angola © SADC
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unaelezwa ulitatizwa kwa sababu za kiufundi, na sasa wakuu hao wanajiandaa kukutana ana kwa ana siku ya Jumamosi, jijini Luanda nchini Angola, kuendeleza mazungumzo hayo.

Lengo kuu la mkutano huo, itakuwa kuthathmini maandalizi ya kutumwa kwa kikosi cha SADC Mashariki mwa DRC kusaidia kupambana na waasi, baada ya hatua hiyo kukubalika mwezi Mei.

Wakuu hao pia waliwahi kukutana na siku za awali kujadili hali ya usalama mashariki ya DRC
Wakuu hao pia waliwahi kukutana na siku za awali kujadili hali ya usalama mashariki ya DRC © LUSA

Afisa wa serikali ya DRC amesema, kikosi cha SADC kinatarajiwa kuwasili nchini DRC ndani ya wiki kadhaa zijazo, baada ya nchi za Afrika Kusini, Malawi na Tanzania, kutangaza kuonesha utayari wa kutuma wanajeshi wao.

Inatarajiwa kuwa, mkutano huo wa Jumamosi, utaidhinishwa rasmi kutumwa kwa kikosi hicho baada ya vikao kadhaa vya wakuu wa majeshi,na hii inakuja baada ya Kinshasa kusema muda wa kikosi cha pamoja cha nchi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kinafika mwisho mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.