Wakuu wa nchi za SADC wanakutana kujadili usalama wa mashariki ya DRC
Nairobi – Wakuu wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC wanakutana kwa dharura jijini Luanda nchini Angola, kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Mkutano huo unafuatiwa na ule uliofanyika mapema wiki hii kwa njia ya video, kuthathmini maandalizi ya kutumwa kwa kikosi maalum cha jeshi kutoka Jumuiya ya SADC kusaidia kupambana na waasi.
Thanked H.E @jlprdeangola for convening today’s virtual Extraordinary #SADC Summit, where we discussed a range of topics including finding a lasting solution to the ongoing security situation in Eastern #DRC. 🌍 #SAMIDRC pic.twitter.com/zUcij5fsHO
— Hakainde Hichilema (@HHichilema) October 31, 2023
Hatua hiyo ilikubaliwa wakati wa kikao cha kwanza cha wakuu hao wa nchi, kilichofanyika mwezi Mei, lakini kumekuwa na mchakato wa miezi kadhaa kuunda kikosi hicho.
Kuelekea mkutano huu, afisa wa serikali ya DRC amesema, kikosi cha SADC kinatarajiwa kuwasili Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya mataifa matatu ya Afrika Kusini, Malawi na Tanzania, kuonesha utayari wa kutuma wanajeshi wao.
Serikali ya Kinshasa, ambayo imesema kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki hakijafanya vya kutosha kumaliza makundi ya waasi hasa M 23, imekuwa ikishinikiza ujio wa kikosi cha SADC kuelekea kumalizika kwa muda wa kikosi cha EAC mwezi Desemba.