Pata taarifa kuu

DRC : Ujumbe wa SADC kutamatisha ziara yake ya wiki moja siku ya Ijumaa

Nairobi – Ujumbe wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC kuthathmini utayari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuelekea uchaguzi mkuu wa Desemba, unatamatisha ziara yake ya wiki moja siku ya Ijumaa.

Kazi kubwa ya ujumbe huo ni kuthathmini utayari wa DRC kuelekea uchaguzi huo
Kazi kubwa ya ujumbe huo ni kuthathmini utayari wa DRC kuelekea uchaguzi huo CIA world factbook
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inaelekea kufikia tamati baada ya serikali ya DRC mwezi Julai, kuomba Jumuiya ya SADC kutuma waangalizi wake wakati wa uchaguzi huo wa Desemba.

Wajumbe hao wamekuwa wakikutana na vyama vya siasa na wadau wengine wanaohusika na maandalizi ya uchaguzi huo,wakiwemo maafisa wa Tume ya uchaguzi CENI.

Kazi kubwa ya ujumbe huo ni kuthathmini utayari wa DRC kuelekea uchaguzi huo.

Kwanza ni kuthathmini iwapo mazingira ya kisiasa na usalama yanaruhusu kufanyika kwa uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

Aidha, wajumbe hao wanathathmini utayari wa tume ya uchaguzi CENI kusimamia uchaguzi huo. Baada ya ziara hiyo, ujumbe huo unatarajiwa kutoa ripoti yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.