Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Liberia: Wito wa utulivu watolewa kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais

Liberia inasubiri matokeo baada ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais ya Jumanne, Novemba 14. Rais anayemaliza muda wake, George Weah, anakabiliana na aliyekuwa makamu wa rais wa Ellen Johnson Sirleaf, Joseph Boakai. Katika duru ya kwanza, wagombea hao wawili walikaribina kura: kulikuwa na tofauti ndogo ya kura 7,000 kati ya wawili hawa. Katika hali kama hiyo, matokeo yanasubiriwa kwa hamu. Na ECOWAS, kama Umoja wa Mataifa, wameongeza kutoa wito wa utulivu.

Watu wakiwa kwenye foleni ili kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais huko Monrovia, Liberia, Novemba 14, 2023.
Watu wakiwa kwenye foleni ili kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais huko Monrovia, Liberia, Novemba 14, 2023. AP - Rami Malek
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Monrovia, Bineta Diagne

Jumatano asubuhi, makumi ya watu wanaomuunga mkono Joseph Boakai walionyesha furaha yao karibu na eneo la Congo Town. Tangu uchaguzi wa Jumanne, Joseph Boakai hajazungumza. Chama chake hakijatoa taarifa yoyote. Lakini makada wenye ushawishi mkubwa wa Chama cha Unity, huhamasisha wafuasi wao na kusambaza matokeo yasiyo rasmi kwenye mitandao ya kijamii.

Ujumbe wa waangalizi wa ECOWAS unaonyesha "wasiwasi wake mkubwa kuhusu kauli za uchochezi na mikutano ya waandishi wa habari iliyopangwa na vyama vya siasa kutangaza matokeo kabla ya wakati," ECOWAS imesema katika taarifa. ECOWAS inavitaka vyama vya siasa kutulia na kuvitaka visubiri kutangazwa rasmi kwa matokeo.

Kwa upande wake, NEC, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ilianza mchakato wa kukusanya matokeo hayo Jumatano. Kwa sasa, ni 22% pekee ya kura zilizopigwa. Kwa mujibu wa sheria, NEC ina siku 15 kutangaza matokeo. "Tunajitahidi kupunguza muda wa kusubiri," anahakikisha Davidetta-Brown Lansana,Mwzenyekiti wa NEC. "Tulitekeleza mchakato wa uadilifu," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.