Pata taarifa kuu

Raia wa Liberia kushiriki duru ya pili ya uchaguzi wa urais wiki ijayo

Nairobi – Raia wa Liberia, wanatarajia kurejea tena kwenye sanduku la kura Jumanne ya wiki ijayo, kuchagua kati ya rais George Weah au makamu wa rais wa zamani, Joseph Boakai, baada ya duru ya kwanza wagombea hawa kutofikisha asilimia 50 ya kura zote.

Uchaguzi wa Liberia
Baada ya matokeo ya duru ya kwanza, George Weah alipata asilimia 43.83 ya kura zote huku mpinzani wake Joseph Boakai, yeyé akipata asilimia 43.44 ya kura zote REUTERS - CARIELLE DOE
Matangazo ya kibiashara

Baada ya matokeo ya duru ya kwanza, George Weah alipata asilimia 43.83 ya kura zote huku mpinzani wake Joseph Boakai, yeyé akipata asilimia 43.44 ya kura zote na kuwalazimisha kwenda kwenye duru ya pili.

Tofauti ndogo ya kura walizopata kwenye duru ya kwanza na kutoshiriki kwa mgombea aliyeshika nafasi ya tatu kwenye uchaguzi huo, kunamaanisha kuwa uchaguzi wa wiki ijayo utakuwa wa ushindani mkubwa.

George Weah wakati akikubali matokeo ya uchaguzi alisema raia wa Liberia ndio wameshinda katika uchaguzi huo
George Weah wakati akikubali matokeo ya uchaguzi alisema raia wa Liberia ndio wameshinda katika uchaguzi huo © AFP

Uchaguzi wa Jumanne ijayo ni kama marudio ya ilivyokuwa mwaka 2017, ambapo baada ya duru ya pili, Weah alimshinda Boakai kwa kupata ushindi wa asilimia 61.54, wengi wa waliomchagua waki wa Vijana ingawa safari hii wameonesha kutokuwa na Imani nae tena.

Joseph Boakai, ndiye rais mteule wa Liberia.
Joseph Boakai, ndiye rais mteule wa Liberia. © Bineta Diagne / RFI

Wagombea wote tayari wamepata uungwaji mkono kutoka kwa vyama vilivyoshindwa kwenye duru ya kwanza, huku wakiahidi kutatua mdororo wa uchumi unaoikabili nchi hiyo, Weah akilaumu athari za mlipuko wa uviko19 na vita ya Urusi na Ukraine kushindwa kutimiza ahadi zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.