Pata taarifa kuu

Raia wa Liberia wanashiriki duru ya pili ya uchaguzi wa urais

Nairobi – Raia nchini Liberia wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais, mchezaji soka wa zamani na ambaye ndiye rais wa sasa George Weah akipambana na mwanasiasa mkongwe Joseph Boakai.

Tume ya uchaguzi ina siku 15 kuchapisha matokeo ya uchaguzi lakini pia inauwezo wa kufanya hivyo mapema
Tume ya uchaguzi ina siku 15 kuchapisha matokeo ya uchaguzi lakini pia inauwezo wa kufanya hivyo mapema AP - Rami Malek
Matangazo ya kibiashara

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika tarehe 10 ya mwezi Oktoba, rais Weah mwenye umri wa miaka 57 na mpizani wake wa karibu Boakai mwenye umri wa miaka 78, walipata zaidi ya asilimia 43 ya kura zote, Weah akiongoza kwa kura  7,126.

Uchaguzi wa mwaka huu ndio wa kwanza tangu Umoja wa Mataifa kumaliza mpango wake wa kulinda amani nchini Liberia mwaka wa 2018.

Rais George Weah anakabiliwa na upizani mkali kutoka kwa mwanasiasa mkongwe Joseph Boakai
Rais George Weah anakabiliwa na upizani mkali kutoka kwa mwanasiasa mkongwe Joseph Boakai AFP - AHMAD GHARABLI,SEYLLOU

Umoja wa Mataifa uliwatuma wanajeshi wake nchini humo baada zaidi ya watu 250,000 kuawawa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka wa 1989 na 2003.

Zaidi ya wapiga kura milioni 2.4 wamesajili kushiriki zoezi hilo, vituo vya kupiga kura vikiwa vimefunguliwa saa mbili asubuhi na vinatarajiwa kufungwa saa kumi na mbili jioni.

Rais George Weah, anawania muhula wa pili
Rais George Weah, anawania muhula wa pili REUTERS - CARIELLE DOE

Rais Weah amepata ushawishi baina ya vijana kwenye taifa hilo wakati mpizani wake Boakai mwanasiasa mkongwe akiwa na tajiriba katika utumishi wa umma na sekta ya kibinafsi.

Tume ya uchaguzi ina siku 15 kuchapisha matokeo ya uchaguzi lakini pia inauwezo wa kufanya hivyo mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.