Pata taarifa kuu

Liberia: UN yatoa wito wa kudumishwa kwa amani kulekea duru ya pili ya uchaguzi

Raia nchini Liberia wanatarajiwa kupiga kushiriki duru ya pili ya uchaguzi wa urais Jumanne ijayo katika kinyang'anyiro kikali kati ya rais George Weah na mwanasiasa wa upinzani wa Joseph Boakai.

Rais Weah anawania kuongoza taifa hilo kwa muhula wa pili
Rais Weah anawania kuongoza taifa hilo kwa muhula wa pili REUTERS - CARIELLE DOE
Matangazo ya kibiashara

Kuelekea uchaguzi huo wa Jumanne, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande husika katika uchaguzi huo kuhakikishia unafanyika kwa njia ya amani.

Huu ni ndio uchaguzi wa kwanza katika taifa hilo la Afrika Magharibi tangu kuondoka kwa walinda amani wa umoja wa mataifa.

Weah, 57, na Boakai, 78, walikosa kupata kura zinazohitajika ilikutangazwa mshindi wa urais kwenye taifa hilo katika uchaguzi wa Oktoba 10.

Rais George Weah, anawania muhula wa pili
Rais George Weah, anawania muhula wa pili REUTERS - CARIELLE DOE

Katika uchaguzi wa mwezi jana Weah alipata asilimia 43.83 ya kura zote dhidi ya Boakai 43.44.

Baadhi ya wapiga kura nchini humo wanamtuhumu rais Weah kwa kushindwa kukabiliana na ufisadi na kuboresha maisha ya watu maskini zaidi huku kukishuhudiwa kupanda kwa bei na uhaba wa mahitaji muhimu.

Boakai alikuwa makamu wa rais kuanzia 2006 hadi 2018 chini ya Ellen Johnson Sirleaf, rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuchaguliwa.

Joseph Boakai, ndiye rais mteule wa Liberia.
Joseph Boakai, ndiye rais mteule wa Liberia. © Bineta Diagne / RFI

Makamu huyo wa rais wa zamani anasema chama chake cha Unity kinataka kunusuru raia nchi kutoka kwa utawala mbovu na ufisadi.

Boakai pia ameahidi kuboresha miundombonu, kuwekeza katika sekta ya kilimo na kubadilisha mtazamo wa taifa hilo katika majukwa ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.