Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Burkina Faso: Mamlaka yatangaza vifo visivyopungua 70 kuhusiana na mauaji ya Zaongo

Nchini Burkina Faso, taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka ya Burkina Faso ilitolewa siku ya Jumatatu usiku, Novemba 13, kuhusu mauaji ya Zaongo. Wilaya hii ya kaskazini-kati mwa Burkina ilikumbwa na shambulio baya zaidi wiki moja iliyopita, na hivyo kuharibu kabisa kijiji kizima.

Maafisa wa jeshi la Burkina Faso wakipiga doria karibu na gari la kivita la Ufaransa lililoegeshwa Kaya, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini-kati wa Burkina Faso, mnamo Novemba 20, 2021.
Maafisa wa jeshi la Burkina Faso wakipiga doria karibu na gari la kivita la Ufaransa lililoegeshwa Kaya, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini-kati wa Burkina Faso, mnamo Novemba 20, 2021. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Ni baada ya siku nane ambapo taarifa rasmi ya kwanza iliyobainisha mauaji ya Zaongo ilitolewa. Taarifa iliyotiwa saini na Mwendesha Mashtaka wa Brukina Faso, inabaini kwamba ripoti ya kwanza kuhusiana na vifo iliyotajwa kuwa ya muda inaeleza vifo vya watu 70 katika kijiji hiki katika cha Kaskazini.

Waathiriwa hasa ni watoto na wazee, wanaume na wanawake. Wachunguzi pia wamebaini mali na nyumba vilivyochomwa moto au kuharibiwa na washambuliaji. Kwa mujibu wa timu za ofisi ya mashtaka kwenye eneo hilo, zikiambatana na Kikosi Maalum cha Uchunguzi wa Kupambana na Ugaidi, haiwezekani, kwa sasa, kutambua wahusika wa ukatili huu, kulingana na taarifa kutoka kwa mamlaka, licha ya ushuhuda wa wazazi wa waathirriwa na majeruhi ambao waliweza kutoroka mauaji haya.

Upatikanaji wa kijiji hicho haukuwa rahisi kwani, kwa mujibu wa mwendesha mashitaka, walilazimika kutegua mabomu ya ardhini kwenye barabara inayoelekea kijijini hapo na wapelelezi, wanaoundwa na kikosi maalum cha uchunguzi wa kupambana na ugaidi, walijibu mashambulizi dhidi ya msafara huo. 

Mwezi Aprili mwaka huu, huko Karma, kaskazini mwa Burkina Faso, mauaji mengine yalighadhabisha mamlaka ya nchi hiyo na pia jumuiya ya kimataifa. Wakati huo, watu 136, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, waliuawa na watu waliovalia sare za vikosi vya jeshi. Serikali ya mpito pia ilianzisha uchunguzi huko Karma. Matokeo ya uchunguzi huu bado hayajajulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.