Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Wanajeshi 53 wa vikosi vya usalama wauawa katika shambulio la wanajihadi

Nairobi – Taarifa za jeshi nchini Burkina Faso zimesema kuwa wapiganaji 53, wakiwemo wanajeshi 17 na wasaidizi wa jeshi (VDP) 36 , wameuawa wakati wa shambulio la watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Koumbri, nchini Burkina Faso.
Koumbri, nchini Burkina Faso. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Tarkribani wanachama 30 wa vikosi vya usalama walijeruhiwa katika shambulo hilo.Aidha jeshi linasema kuwa washambuliaji kadhaa wamethibitiwa katika operesheni ya kukabiliana  na zana zao za vita kuharibiwa huku oparesheni ikizidi kuendelea katika eneo hilo.

Kikosi kilichoshambuliwa ni sehemu ya kikosi cha 12 cha askari wa nchi kavu, ambao kambi yao iko Ouahigouya, katika jimbo la Yatenga. Ilikuwa kama kilomita ishirini kaskazini mwa kambi yao, katika mji wa Koumbri hasa, ambapo askari walishambuliwa. Mbali na wapiganaji 53 waliouawa, thelathini waliojeruhiwa katika safu ya jeshi,walisafiriswa katika hospitali na kupewa huduma ya mwanzo.

Operesheni ambayo wanajeshi hao walikuwa wakiendesha Koumbri ilielezewa kuwa ya "ujasiri". Kwa hakika lilikuwa ni suala la kulinda eneo hilo naviunga vyake, eneo lililo chini ya udhibiti wa makundi ya kigaidi. Na kuwezesha raia waliotoroka makaazi yao kurudi.

Shambulio hilo bado halijadaiwa na washambuliaji au kuhusishwa na kundi maalum. Lakini kulingana na jeshi, "magaidi kadhaa" waliokuwa mafichoni  wameangamizwa na vifaa vyao viliharibiwa. Na operesheni za kujibu mashambulizi yao bado zinaendelea katika eneo hilo.

Tangu mwaka 2015 zaidi ya raia 16,000 wanajeshi na pilisi wameuwawa katkka mashambulio ya wanajihadi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.