Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Burkina Faso: 'magaidi' wasiopungua 65 aangamizwa magharibi, jeshi latangaza

Vikosi vya jeshi vya Burkina Faso vimetangaza kuwa vimewaangamiza, kuanzia Agosti 7 hadi Septemba 1, 2023, angalau "magaidi" 65 wakati wa operesheni katika majimbo kadhaa. Kufuatia operesheni hii iliyoongozwa na kikosi cha 7 cha uingiliaji kati wa haraka, watu ambao walikuwa wametoroka makaazi yao waliweza kurudi katika vijiji vyao, kwa mujibu wa jeshi.

Kapteni Ibrahim Traoré, wakati wa mkutano na Vladimir Putin karibu na Saint Petersburg, Julai 29, 2023.
Kapteni Ibrahim Traoré, wakati wa mkutano na Vladimir Putin karibu na Saint Petersburg, Julai 29, 2023. AFP - ALEXEY DANICHEV
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Majeshi amekaribisha operesheni hii ambayo, kulingana naye, inadhoofisha sana makundi ya kigaidi yenye silaha magharibi mwa Burkina Faso. Operesheni hiyo ilitayarishwa "kwa uangalifu" na kutekeezwa kufuatia habari maalum, chanzo hicho kinaelezea.

Wakati wa mapigano, watano waliojeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watu wawili wa kujitolea kwa ajili ya ulinzi wa taifa, ambao wamerekodiwa ndani ya jeshi la Burkina Faso.

Kikosi cha 7 cha uingiliaji kati wa haraka kilifanya mashambulizi kwenye maeneo kadhaa ya kigaidi katika majimbo ya Kénédougou, Houet na katika eneo la Cascades, kulingana na jeshi. Operesheni hii ilifanya iwezekane "kuwatimu magaidi" katika maeneo kadhaa kama vile Ouangolodougou, Konkala, Bolibana na Diarakorosso, yote yaliyo katika ukanda wa magharibi ya nchi.

"Ripoti iliyokusanywa kwa operesheni mbalimbali inaonyesha zaidi ya magaidi 65 waliangamizwa," linabainisha jeshi la Burkina Faso. Kiasi kikubwa cha silaha, risasi, vyakula, magari na vifaa vya mawasiliano pia vilikamatwa.

Operesheni hii, kulingana na makao makuu ya jeshi, ilifanya iwezekane kutekeleza hatua kadhaa kwa manufaa ya watu ambao walikuwa chini ya unyanyasaji na makundi haya ya kigaidi yenye silaha. Raia wamehamishwa katika baadhi ya maeneo, umeme na mitandao ya simu imerejeshwa.

Kumbuka pia kwamba afisa wa polisi na watu wanne wa kujitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi waliuawa siku ya Ijumaa Septemba 1, baada ya mapigano dhidi ya makundi yenye silaha katika eneo la Silmiougou, eneo la Centre-North. Karibu magaidi kumi waliangamizwa, kulingana na jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.