Pata taarifa kuu

Niger yaidhinisha Mali na Burkina kutuma wanajeshi wao iwapo kutatokea shambulio

Utawala wa kijeshi nchini Niger umeidhinisha Mali na Burkina Faso kutuma wanajeshi wao kwenye ardhi ya Niger iwapo kutatokea shambulio, nchi hizo tatu zilitangaza katika taarifa ya pamoja siku ya Alhamisi, zikipendekeza kwamba viongozi wa mapinduzi wanakusudia kupinga shinikizo kutoka nje la kurejesha utawala wa kikatiba.

Jenerali Tiani, mkuu wa mapinduzi nchini Niger, wakati wa hotuba yake ya televisheni kwenye kituo cha Télé Sahel, Agosti 19, 2023.
Jenerali Tiani, mkuu wa mapinduzi nchini Niger, wakati wa hotuba yake ya televisheni kwenye kituo cha Télé Sahel, Agosti 19, 2023. © ORTN
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linakuja wakati Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ikitishia kuingilia kijeshi nchini Niger ili kurejesha utawala wa kikatiba baada ya jeshi kumpindua rais Mohamed aliyechaguliwa kidemokrasia mwishoni mwa mwezi Julai. Nchi hizo zilikumbusha kuwa Mali na Burkina Faso zitachukulia uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Niger kuwa tangazo la vita dhidi yao.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ilijaribu kufanya mazungumzo na viongozi wa mapinduzi, lakini ikaonya kuwa iko tayari kutuma wanajeshi Niger kurejesha utawala wa kikatiba ikiwa juhudi za kidiplomasia zitashindwa.

Ongezeko lolote la uhasama au vita linahatarisha zaidi usalama katika eneo hilo linalokabiliwa na waasi kwani majirani wa Niger, Mali na Burkina Faso zinazotawaliwa na wanajeshi kupitia mapinduzi wamesema wataunga mkono Niger katika mzozo wowote na ECOWAS.

Siku ya Alhamisi, mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi hizo tatu washirika, walisema walikutana katika mji mkuu wa Niger, Niamey, kujadili kuimarishwa kwa ushirikiano wa kiusalama na masuala mengine yanayowahusu.

Taarifa hiyo ilisema mawaziri hao walikaribisha kutiwa saini siku ya Alhamisi na mkuu wa serikali ya Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, kwa sheria mbili "zinazoidhinisha vikosi vya ulinzi na usalama vya Burkina Faso na Mali kuingilia kati nchini Niger.

"Mawaziri wa Burkina Faso na Mali walisisitiza kukataa kwao kuingilia kijeshi dhidi ya raia wa Niger hatua ambayo itachukuliwawa kama tangazo la vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.