Pata taarifa kuu

ECOWAS yaendelea na maandalizi yake kwa uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Niger

Wakati diplomasia ikishika kasi na kwamba sauti za kupinga uingiliaji kati wowote wa kijeshi wa ECOWAS nchini Niger zimesikika baada ya mkutano wa wakuu wa majeshi, jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi halijatupili mbali hata kidogo chaguo la kuingilia kati kijeshi kurejesha demokrasia nchini Niger na rais Mohammed Bazoum kweye nafasi yake. 

Mkuu wa Majeshi wa Ghana, Makamu Admirali Seth Amoama (katikati), akiwa karibu na Mkuu wa majeshi wa Gambia Luteni Jenerali Yankuba Drammeh (kushoto), na Mkuu wa majesjhi wa Côte d'Ivoire Jenerali Lassina Doumbia, wakati wa mkutano usio wa kawaida wa Wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa ECOWAS, mjini Accra, Agosti 18, 2023.
Mkuu wa Majeshi wa Ghana, Makamu Admirali Seth Amoama (katikati), akiwa karibu na Mkuu wa majeshi wa Gambia Luteni Jenerali Yankuba Drammeh (kushoto), na Mkuu wa majesjhi wa Côte d'Ivoire Jenerali Lassina Doumbia, wakati wa mkutano usio wa kawaida wa Wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa ECOWAS, mjini Accra, Agosti 18, 2023. © Richard Eshun Nanaresh / AP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vya karibu, mchakato unaendelea. Mipango hiyo, ambayo iliidhinishwa mjini Accra na kwa sasa inatoa nafasi ya kutumwa kwa wanajeshi, inaendelea.

Viongozi wa kijeshi wa kikosi cha dharura wako tayari kutuma vikosi vyao nchini Niger, huku wakisema, "hatujapokea amri ya kupinga"  kuingilia kijeshi nchini Niamey, kulingana na afisa mkuu. Kwa kwelii, chaguo la kuingilia kijeshi kurejesha utawala wa kikatiba nchini Niger bado ni muhimu, liko na linapangwa, anaripoti mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, wakuu wa majeshi kwa sasa wanasimamia zoezi la kupelekwa kwa wanajeshi hao. Katika awamu hii ya uanzishwaji, nchi zilizo mbali na Niger zimekubali kutuma wanajeshi wao katika nchi zinazopakana na Niger, zilizochaguliwa kama ngome. Hatua hii iko karibu, kulingana na duru za kuaminika: wanajeshi na vifaa wanaweza kusafirishwa kwa njia ya anga au baharini.

Taarifa za hivi punde zinaonyesha kuwa kikosi cha dharura cha ECOWAS kitaundwa na wanajeshi kutoka Benin, Nigeria, Senegal, Côte d'Ivoire, Guinea-Bissau, na sasa unazungumziwa mchango wa Ghana. Ili kuashiria kujitolea kwake, Ghana iliandaa mkutano wa Wakuu wa Majeshi mnamo Agosti 18 na rais wake Nana Akoufo Ado aliwapokea maafisa wakuu waliohudhuria kwa takriban dakika arobaini.

Nchi nyingine zilizotoa ahadi huko Accra zinaweza kukamilisha idadi ya kikosi hiki jeshi la kusubiri la ECOWAS.

"Tutafanya kazi, hakuna haja ya mkutano mwingine, tuko tayari"

Miito ya suluhu kupitia njia za kidiplomasia na tangazo la ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria - inayopinga matumizi ya nguvu kurejesha utawala wa kikatiba - haionekani kupunguza kasi ya chaguo la kijeshi.

Wengi wa washiriki tayari wameweka makao yao makuu: huu utakuwa utaratibu wa amri ya uendeshaji. Uratibu utafanyika mara moja kwenye ngome kuu. "Tunajua jinsi ya kufanya hivyo," amesema afisa mmoja mkuu, ambaye hakutaja siku ya kuanza kwa operesheni. "Tutafanya kazi hiyo, [hakuna] haja ya mkutano mpya, tuko tayari", amebaini afisa mkuu wa jeshi katika kanda hiyo.

AU ilitaka kupinga uingiliaji kati wa kijeshi, bila "kupinga ECOWAS"

Katika ngazi ya kidiplomasia, Umoja wa Afrika umechukua muda kujieleza waziwazi kuhusu maamuzi ya ECOWAS. Taarifa yake kwa vyombo vya habari ya Jumanne Agosti 22 inashuhudia utata wa hali hiyo: ikiwa umoja huo unataka kurejea kwa utawala wa kikatiba na kuunga mkono vikwazo, unaonyesha upendeleo wake kwa diplomasia bila kupinga kabisa chaguo la kijeshi ili "kutotofautiana na ECOWAS" , kulingana na Pape Ibrahima Kane, mtaalamu katika taasisi za Kiafrika katika Wakfu wa Open Society Africa (OSIWA).

AU imesitisha ushiriki wa Niger katika shughuli zake, na hivyo inazingatia ukweli kwamba Rais Bazoum amepinduliwa na mapinduzi "yamekamilika".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.