Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-DPLOMASIA

Mapinduzi Niger: ECOWAS kukutana Alhamisi hii wakati mazungumzo na wanajeshi yamekwama

Wakuu wa nchi za Afrika Magharibi wanatarajiwa Alhamisi hii kwa mkutano usio kuwa wa kawaida wa ECOWAS. Suala moja tu litakuwa kwenye ajenda: hali nchini Niger. Viongozi hao watalazimika kufanya chaguo, siku kumi baada ya mapinduzi, kati ya mazungumzo au operesheni ya kijeshi.

Mwanajeshi wa Nigeria akiwa mbele ya majengo ya ECOWAS mjini Abuja, Nigeria.
Mwanajeshi wa Nigeria akiwa mbele ya majengo ya ECOWAS mjini Abuja, Nigeria. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Je, wakuu wa nchi za Afrika Magharibi watatangaza operesheni ya kijeshi? Au kutangaza maendeleo makubwa katika mazungumzo yao na serikali ya Niger? Matarajio ya operesheni ya kijeshi kwa kweli yanaonekana kupungua, lakini askari walioko Niamey bado wameikaa imara kwa kujiandalia kukabliana na mashambulizi yoyote yanayoweza kutokea kwenye ardhi yao kutoka vikosi vya ECOWAS.

Kwa hatua zozote, ECOWAS inapitia wakati mgumu wakati majaribio yake ya mara kwa mara ya kuelezea njia ya Niger kuondokana na mzozo huo yanaonekana kugonga mwamba. Uwepo wenyewe wa ECOWAS uko hatarini, kulingana na rais wa Guinea-Bissau.

"Hali ni ngumu kwa ECOWAS kwa sababu shinikizo linaongezeka waziwazi kati ya ECOWAS na mamlaka ya kijeshi ncini Niger tangu mapinduzi yaliyomimua mamlakani rais wa Niger Mohamed Bazoum, " amesema rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo.

'Hakuna chaguo ambalo limekataliwa'

Kutokana na  vikwazo vya kiuchumi, jeshi lililo madarakani huko Niamey lilipinga kuanzisha mazungumzo. Ujumbe wa kwanza wa Nigeria ulilazimika kurudi nyuma wiki iliyopita, kisha ujumbe wa pamoja wa ECOWAS, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenda Niger kwa mazungumzo na wanajeshi wanaoshikilia madaraka ulikataliwa Jumatatu jioni.

Hata hivyo, bado kuna matumaini ya kufikia muafaka. Siku ya Jumatano, amiri wa zamani wa Kano na gavana wa zamani wa benki kuu ya Nigeria, Lamido Sanusi anayeheshimika sana nchini Nigeria, aliweza kukutana na Jenerali Abdourahamane Tchiani huko Niamey. "Nilikuja nikitumaini kwamba ziara yangu inaweza kufungua njia ya mazungumzo. Nilikuwa na mazungumzo ya dhati na ya kujenga na Jenerali Tchiani na nilirudi kukutana na rais wa Nigeria kumfikishia taarifa kamili kuhusiana na mazungumzo yangu na kiongozi wa mapinduzi nchini Niger,” almesema Lamido Sanusi, ambaye alieleza kuwa yeye si mjumbe wa serikali ya nchi yake.

Mkutano huo utafunguliwa na kufungwa kwa hotuba ya Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu, mkuu wa sasa wa ECOWAS, ambaye anakabiliwa na upinzai mkubwa kutoka kwa wanajesi wanaoshikilia mamlaka nchini Niger, Mali, Burkina Faso, na Guinea. Rais Bola Tinubu amesisitiza tena kwamba mazungumzo yamesalia kuwa "njia bora zaidi" lakini "hakuna chaguo ambalo limekataliwa", amesema msemaji wake.

Hata hivyo msimamo wa Senegal ni kushikiza wanajrshi wanaoshikilia mamlaka nchini Niger kurejesha utaratibu wa kikatia na kumuachilia rais Mohamed Bazoum na kumrejesha kwenye wadhifa wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.