Pata taarifa kuu

Niger: Mkutano wa wakuu wa majeshi wa ECOWAS uliopangwa kufanyika Jumamosi waahirishwa

Wakuu wa majeshi ya nchi za ECOWAS ambao walitarajiwa kukutana Jumamosi hii mjini Accra kujadili kuhusu uwezekano wa kupelekwa kwa kikosi cha dharura cha ECOWAS nchini Niger. Mkutano huo hatimaye umeahirishwa kwa "sababu za kiufundi".

Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wakikutana mjini Abuja kujadili hali nchini Niger, Agosti 10, 2023.
Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wakikutana mjini Abuja kujadili hali nchini Niger, Agosti 10, 2023. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan

Hatimaye, Wakuu wa majeshi ya ECOWAS hawatakutana kama ilivyopangwa Jumamosi hii mjini Accra kwa "sababu za kiufundi". Baadhi ya wajumbe wana shida kufika mji mkuu wa Ghana kwa wakati kwa sababu safari za ndege za kibiashara zinazotolewa haziwiani na njia inayotakiwa.

Wakuu wa majeshi walipaswa kukutana ili kuanzisha "kikosi cha dharura" cha jumuiya ya Afrika Magharibi kwa ajili ya kurejesha utaratibu wa kikatiba nchini Niger, uamuzi uliochukuliwa na ECOWAS katika mkutano wa kilele wa Agosti 10 huko Abuja.

Duru za kuaminika zinasema mkutano huo wa unatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo. Tarehe inasalia kubainishwa na kuthibitishwa, lakini hii haipaswi kuchelewesha mchakato wa kuanzishwa kwa kikosi hiki kwa lego la kweda kurejesha utawala wa kikatiba nchini Niger.

Wakuu wa majeshi wa Benin, Côte d'Ivoire, Ghana na Nigeria walikuwa na vikao vya kazi Ijumaa hii, baadhi walikutana ana kwa ana, wengine walifanya mikutano ya mtandaoni. Kwa mujibu wa habari zetu, idadi ya wanajeshi wa kikosi hiki imeongezeka kutokana na nchi zingine kutangaza kwamba zitachangia kwa wanajeshi kama vile Guinea-Bissau.

Pia taarifa tunazo ni kwamba nchi hizi zitaweka askari wao kwa fedha zao wenyewe. Rais wa Côte d'Ivoire Allassane Ouattara hili mwishoni mwa mkutano wa Abuja, na kutangaza kwamba "marekebisho ya bajeti yatafanywa ili vikosi vyetu na maafisa wetu wanaoshiriki katika operesheni hii ya kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Niger wasikose wanachohitaji".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.