Pata taarifa kuu
MAHOJIANO-DIPLOMASIA

Catherine Colonna: 'Viongozi wa mapinduzi Niger wana hadi kesho kukabidhi madaraka'

Mkutano ulifanyika Jumamosi hii asubuhi Agosti 5 kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna na Waziri Mkuu wa Niger Ouhoumoudou Mahamadou kuhusu hali ya Niger, baada ya mapinduzi ya Julai 26. Muda unayoyoma, kwa sababu kesho Jumapili ni muda wa mwisho wa ECOWAS.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna. © AFP / BENOIT TESSIER
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Afrika Magharibi iliwapa viongozi wa mapinduzi siku saba kurudisha mamlaka. Jumuiya hiyo sasa linasema liko tayari kwa "uingiliaji kati wa kijeshi unaowezekana" kuwaondoa wanajeshi hao madarakani, wakati rais mteule wa Niger Mohamed Bazoum bado anazuiliwa katika makazi yake. Katika mahojiano na RFI, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amewataka wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Niger kuachia madaraka. Fuata mahojiano.

RFI : Ulikutana na Waziri Mkuu wa Niger, kuna maamuzi yoyote mliochukuwa na alikupa habari yoyote kutoka kwa Rais Bazoum?

Catherine Colonna : Hakika nimekutana na Waziri Mkuu wa Niger ambaye yuko Paris, kwa vile hakuweza kurejea nchini mwake. Alikuwa Italia wakati wa jaribio la mapinduzi, kuiwakilisha Niger katika mikutano ya kimataifa: mkutano wa usalama wa chakula, ambao ulifanyika Roma. Anawakilisha serikali halali ya Niger na ni afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Niger, kama vile rais aliyechaguliwa kidemokrasia, ambaye ni Rais Bazoum. Kwa hivyo mimi na Waziri Mkuu tumezungumza hivi punde ili kubadilishana fikra, ili kutambua kwamba jumuiya ya kimataifa ina kauli moja, kama nchi za eneo hilo, katika kulaani jaribio hili, kulaani mapinduzi haya yanayoongozwa na askari wachache nchini Niger. Na kudai kurejeshwa mara moja kwa utaratibu wa kikatiba, kudai kurejeshwa kwa demokrasia nchini Niger na kuendana na madai haya ya wazi kabisa, kwa upande mmoja, hatua ambazo tayari zimetumika na ECOWAS, na pia, zikiambatana na tarehe ya mwisho, tishio ambalo lazima lichukuliwe kwa uzito mkubwa wa kuingilia kati kwa jeshi la kikanda ikiwa wanajeshi hao wa Niger hawakusikiza matakwa ya Wakuu wa Nchi za ECOWAS, na hawakupaswa kurejesha demokrasia mara moja, yaani ndani ya muda wa siku saba, ambao unaisha kesho Jumapili.

RFI : Je, Ufaransa inaunga mkono uingiliaji kati huu kwa usahihi? Je, Ufaransa itahusika katika operesheni hii?

Catherine Colonna : Hatupo kwa masuali hayo. Maamuzi ambayo yalichukuliwa na ECOWAS mara baada ya mapinduzi yanajumuisha shinikizo, yanajumuisha ombi la wazi kutoka kwa nchi za ukanda huo, likielekeza lile la jumuiya nzima ya kimataifa, kurejesha utulivu wa kikatiba, kuheshimu matakwa ya watu wa Niger ndani ya siku saba. . Hiyo ni kusema, kwa uwazi, kurejesha mamlaka, yaani wanajeshi warejeshe mamlaka kabla ya Jumapili. Juhudi hizi zinaendelea, hazijakamilika, bado tuko ndani ya muda huu. Ikiwa, kwa kuwa hili ni swali lako, wale waliohusika na jaribio hili la mapinduzi hawatatekeleza ombi lililotolewa na ECOWAS, basi Wakuu wa Nchi zinazohusika wanapaswa kuchukua uamuzi, walibaini uamuzi wao watakaochukuwa . Ninaamini kwamba matarajio ya kuja kwa njia nyingine lazima yachukuliwe kwa uzito sana. Wakuu wa majeshi kutoka kanda hiyo walikutana, wakafanya maandalizi, ifahamike kuwa maandalizi yamefanyika. Kwa hivyo sasa ni wakati wa viongozi wa mapinduzi kuachia ngazi.

RFI : Viongozi wa mapinduzi, hasa, walisitiha mikataba ya kijeshi na Ufaransa. Je, ni kazi gani ya wanajeshi wa Ufaransa leo nchini Niger? Na una hofu kwamba watalengwa na mashambulizi?

Catherine Colonna : Kuwepo kwa vikosi vya Ufaransa nchini Niger kunatokana na makubaliano ambayo yalitiwa saini na mamlaka halali ya nchi hii miaka kadhaa iliyopita, kwa hiyo wako nchini Niger kwa ombi la mamlaka hii halali. Walakini, unajua, narudia, tangu mapinduzi, Ufaransa imesitisha ushirikiano wake, wa kiraia na kijeshi, kwa sababu za wazi, kwa hivyo ushirikiano huu umesitishwa. Bila shaka, hatutambui maamuzi yaliyochukuliwa na viongozi wa mapinduzi, tunatambua tu maamuzi ya mamlaka halali.

RFI : Lakini je, hali hii inatia shaka mfumo wa Ufaransa wa kupambana na ugaidi unaofikiriwa baada ya Barkhane?

Catherine Colonna : Haiko kwenye ajenda, hata kama, narudia, ushirikiano huu ulipaswa kusitishwa, kwa sababu ya jaribio la mapinduzi ambalo limekuwa likiendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa nchini Niger. Takwa la pamoja la jumuiya ya kimataifa ni, narudia tena, kurejesha demokrasia mara moja na kabla ya kumalizika kwa muda ambao umewekwa na nchi za kikanda, ambao unamalizika kesho. Kwa hivyo wana hadi kesho kukabidhi mamlaka, kuachana na maslahi haya ya kibinafsi, na kurejesha demokrasia nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.