Pata taarifa kuu

Niger: Washington yasitisha programu za msaada kwa serikali

Kutokana na hali inayoendelea nchini Niger, misaada kwa nchi hiyo imesitishwa na washirika kadhaa wa kimataifa: Umoja wa Ulaya, Ufaransa na nchi zingine za Ulaya wameamua kusitisha misaada yao kwa Niger. Kwa upande wa Marekani, tishio la kusitishwa kwa msaada limezinduliwa, lakini bado halijaidhinishwa.

Wafuasi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Niger wakikusanyika wakati wa maandamano yaliyoitishwa kupigania uhuru wa nchi hiyo na kuzuwia kuingiliwa na mataifa ya kigeni huko Niamey, Niger, Agosti 3, 2023.
Wafuasi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Niger wakikusanyika wakati wa maandamano yaliyoitishwa kupigania uhuru wa nchi hiyo na kuzuwia kuingiliwa na mataifa ya kigeni huko Niamey, Niger, Agosti 3, 2023. © Sam Mednick / AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Washington, Guillaume Naudin

Uamuzi huo hatimaye umetathminiwa, wiki moja baada ya onyo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Waziri huyu alihusisha kuendelea kwa misaada na kurejeshwa kwa utaratibu wa kidemokrasia. uamuzi huu bado utajadiliwa: sehemu tu ya msaada imesitishwa. Msaada wa chakula na kibinadamu hauhusiki.

Mwaka 2022, Marekani ilitoa msaada wa zaidi ya dola milioni 200 kwa Niger. Kwa mwaka wa fedha wa 2023, ambao utakamilika mwishoni mwa mwezi Septemba nchini Marekani, dola milioni 130 tayari zimetolewa. Upungufu bado ni mkubwa.

Msaada muhimu wa kijeshi

Tangu mwaka 2012, tawala mbalimbali za Marekani zimetoa zaidi ya dola nusu bilioni kuwaanda na kuwafunza wanajeshi ambao wamechukua madaraka huko Niamey. Takriban wanajeshi 1,100 wa Marekani wapo nchini Niger, hasa kwenye kituo cha anga cha Agadez, ambacho ujenzi wake uligharimu zaidi ya dola milioni 100. Ni kambi ya kijeshi pekee ya Marekani barani humo, mbali na ile wa Djibouti. Taarifa kwa vyombo vya habari inabainisha kuwa operesheni za usalama zinaendelea.

Kwa mujibu wa sheria za Marekani, haya yote lazima yasitishwe kufuatia tukio la mapinduzi dhidi ya mamlaka iliyochaguliwa kidemokrasia. Hii bila shaka inaelezea, kwa sehemu, kusita kwa utawala wa Biden kutaja hivo hali ya nchi na kukata kabisa ushirikiano wake na nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.