Pata taarifa kuu

Niger: Jeshi latishia kujibu jaribio lolote kutoka nje kujaribu kuliondoa madarakani

Nairobi – Uongozi wa kijeshi nchini Niger, umetishia kujibu jaribio lolote kutoka nje kujaribu kuwaondoa madarakani, wakati huu muda wa wiki moja, waliopewa na wakuu wan chi za Jumuiya ya ECOWAS kulitaka kurejesha madaraka kwa rais Mohammed Bazoum, ukikaribia kufika mwisho.

Siku ya Alhamisi kulishuhudiwa maandamano ya maelfu ya watu jijini Niamey kuwaunga mkono wanajeshi
Siku ya Alhamisi kulishuhudiwa maandamano ya maelfu ya watu jijini Niamey kuwaunga mkono wanajeshi © AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi Kanali Amadou Abdramane, akizungumza kupitia Televisheni ya taifa, ametoa onyo hilo, wakati huu wakuu wa majeshi kutoka nchi za ECOWAS wakikutana jijini Abuja, wanakojadiliana uwezekano wa kutumia nguvu dhidi ya jeshi la Niger, iwapo rais Bazoum hatarejeshwa madarakani.

Wiki hii, mataifa ya Mali na Burkina Faso ambayo pia yanaongozwa na jeshi, yaliapa kuisaidia Niger, iwapo ECOWAS itatuma kikosi chake kumrejesha rais Bazoum.

Katika hatua nyingine, jeshi nchini Niger, limetangaza kusitisha ushirikiano wake wa kijeshi na nchi ya Ufaransa na kumfukuza balozi wa nchi hiyo, akiwemo yule wa Marekani, Togo na Nigeria.

Siku ya Alhamisi kulishuhudiwa maandamano ya maelfu ya watu jijini Niamey kuwaunga mkono wanajeshi, huku baadhi ya waandamanaji wakipeperusha bendera ya Urusi.

Ufaransa imewaondoa raia wake nchini Niger, huku Marekani na Uingereza zikitangaza mpango wa kuwarejesha nyumbani wafanyakazi wake wanaofanya kazi ubalozini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.