Pata taarifa kuu

Ufaransa imewaondoa raia wake Niger

Nairobi – Serikali ya Ufaransa inasema imewaondoa raia wake 1,079 kutoka nchini Niger na kutangaza kwamba oparesheni ya kuwahamisha raia wake katika taifa hilo la Afrika ya kati imekamilika.

Ufaransa na mataifa mengine ya EU yamewaondoa raia wake nchini Niger
Ufaransa na mataifa mengine ya EU yamewaondoa raia wake nchini Niger REUTERS - STEPHANIE LECOCQ
Matangazo ya kibiashara

Kupitia kwa ukurasa wake wa twitter, waziri wa ulinzi Sébastien Lecornu nchi yake imewaondoa raia wake na kwamba sasa wako salama.

Haya yanajiri wakati huu rais wa Marekani Joe Biden, akitoa wito wa kuachiwa mara moja kwa rais wa Niger Mohamed Bazoum, anayezuiliwa na kwamba demokrasia inafaa kulindwa.

Rais Biden amesema anatoa wito wa kuachiwa kwa kiongozi huyo na familia yake, wito wake ukija ikiwa imepita wiki moja baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi.

Utawala wa Bazoum uliochaguliwa kidemokrasia uliangushwa Julai 26 baada ya walinzi wake kumzuilia katika makazi yake.

Mataifa mengine ya EU nayo pia yameendelea kuwaondoa raia wake nchini Niger, maandamano zaidi yakiwa yamepangwa kufanyika.

Saa chache baada ya Marekani kutangaza inapunguza idadi ya wafanyikazi nchini Niger, Uingereza nayo pia inasema inachukua hatua kama hizo kwa wahudumu katika ubalozi wake mjini Niamey.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.