Pata taarifa kuu

Niger: Tangu mapinduzi, waandishi wa habari wanayanyaswa na kufanyiwa vitisho

Matangazo ya RFI na France 24 yamesitishwa tangu Alhamisi Agosti 3 na serikali ya Niger. Lakini vyombo vya habari vya Ufaransa au vya kigeni sio pekee vinanyanyaswa tangu mapinduzi hayo. Vyombo vya habari vya Niger na wanahabari wao pia wako chini ya shinikizo, kulingana na mashirika yanayolinda waandishi wa habari.

Waandishi wengi wa habari wanaripoti Mapinduzi nchini Niger, wakati mwingine wanajiweka hatarini.
Waandishi wengi wa habari wanaripoti Mapinduzi nchini Niger, wakati mwingine wanajiweka hatarini. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mbali na kusitishwa kwa matangazo ya RFI na France 24 nchini Niger, ni waandishi wa habari wote ambao wameona hali zao za kazi zikizorota nchini humo tangu mapinduzi, iwe ni wa kigeni au wa ndani, anabanisha Sadibou Marong, mkurugenzi wa ofisi  ya shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka, RSF, katika kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.  "Wito wa kuwapiga mawe hadi kifo unaotolewa dhidi ya waandishi wa habari, na mashambulizi ya moja kwa moja dhidi yao, hali hi inasikitisha sana, ameelea Sadibou Marong. Angalau timu mbili za waandishi wa habari za vituo vya televisheni zilikumbwa na mashambulizi kutoka kwa wafuasi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi. Na hivi punde ilionekana baadhi ya waandamanaji wakianza kuwashambulia waandishi wa habari wa kimataifa. "

Waandishi waomba ulinzi kutoka Baraza la Waandishi wa Habari nchini Niger

Redio za kitaifa na televisheni ziko chini ya shinikizo, wanablogu wanatishiwa... Baadhi ya waandishi wa habari, wanaokabiliwa na vitisho nyumbani kwao, wamelazimika kuomba ulinzi kutoka kwa Baraza la waandishi wa habari nchini Niger. “Ilitubidi tufanye utaratibu wa kuwahamisha na kuhakikisha wanarejea katika maisha yao ya kila siku na kuendelea kufanya kazi zao. Mazingira kwa kweli ni mabaya sana na tunatoa wito kwa kila mtu kuzingatia kwamba uhuru wa vyombo vya habari haupaswi kutiliwa shaka”, anasema mwenyekiti wa baraza hilo Ibrahim Harouna.

Umoja wa Waandishi wa Habari wa Vyombo Huru unatoa angalizo kama hilo na kuomba mamlaka ya Niger kulinda usalama wa waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.