Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

Wakuu wa majeshi ya ECOWAS wafafanua 'uingiliaji kati kijeshi unaowezekana' nchini Niger

Mipangilio ya "uingiliaji kati kijeshi unaowezekana" na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) nchini Niger "imefafanuliwa", ametangaza Kamishna wa Masuala ya Kisiasa na Usalama wa ECOWAS, Abdel-Fatau Musah, baada ya mkutano wa wakuu wa majeshi wa kutoka jumluiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi mjini Abuja Ijumaa Agosti 4.

Mtazamo wa jumla wa Kamati ya Wakuu wa majeshi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) tarehe 2 Agosti 2023 mjini Abuja.
Mtazamo wa jumla wa Kamati ya Wakuu wa majeshi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) tarehe 2 Agosti 2023 mjini Abuja. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

"Mambo yote ya uwezekano wa kuingilia kati yalifanyiwa kazi wakati wa mkutano huu, ikiwa ni pamoja na rasilimali muhimu, lakini pia jinsi gani na lini tutapeleka kikosi," Abdel-Fatau Musah amesema baada ya mkutano huo, mkutano wa siku tatu mjini Abuja.

ECOWAS haitafichua kwa viongozi wa mapinduzi lini na wapi itaingilia kati kijeshi, uamuzi ambao utachukuliwa na wakuu wa nchi, amesema Abdel-Fatau Musah.

ECOWAS imeweka vikwazo na kutishia kuingilia kijeshi nchini Niger ikiwa Rais Bazoum hatarejeshwa madarakani ifikapo Jumapili Agosti 6.

ECOWAS ilituma wajumbe kwenda Niamey Alhamisi, Agosti 3, ambako wanajeshi walimpindua rais Mohamed Bazoum, lakini ujumbe wa ECOWAS uliondoka bila kuwepo kwa maendeleo yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.