Pata taarifa kuu

Ujumbe wa Ecowas wakosa kupata suluhu nchini Niger

Ujumbe wa Ecowas uliyopewa jukumu la kutafuta suluhu ya mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, umeondoka nchini humo bila ya kuafikia muafaka.

Ecowas imekuwa ikitaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Niger
Ecowas imekuwa ikitaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Niger REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Wapatanishi hao waliokuwa wameteuliwa na uongozi wa Ecowas, hawakupatana na kiongozi wa kijeshi aliyeoongoza mapinduzi ya rais Mohamed Bazoum.

Jumuiya hiyo tayari imetangaza vikwazo dhidi ya Niger na umetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo rais Bazoum hatarejeshwa madarakani.

Kwa upande wake rais huyo aliyeondolewa kwenye mamlaka ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia kurejesha uongozi uliochaguliwa kidemokrasia.

Bazoum ameonya kuwa ukanda wote wa Sahel unaweza ukaingia chini ya ushawishi wa Urusi.

Uongozi wa kijeshi nchini Niger, umetishia kujibu jaribio lolote kutoka nje kujaribu kuwaondoa madarakani, wakati huu muda wa wiki moja, waliopewa na wakuu wan chi za Jumuiya ya ECOWAS kulitaka kurejesha madaraka kwa rais Mohammed Bazoum, ukikaribia kufika mwisho.

Viongozi hao pia wametangaza kusitisha majukumu ya mabalozi katika nchi nne zikiwemo Nigeria, Togo, Ufaransa na Marekani huku wakikabiliwa na shinikizo la kimataifa kumrejesha kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia waliyemuondoa madarakani wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.