Pata taarifa kuu

Wajumbe wa Afrika Magharibi waondoka Niger bila kukutana na kiongozi wa mapinduzi

Ujumbe wa Afrika Magharibi uliotumwa Niger uliondoka hapo usiku wa Alhamisi kamkia Ijumaa, baada ya saa chache, bila ya kukutana na mkuu wa kiongozi wa utawala wa kijeshi ambaye alitaka kuvunja ushirikiano wake wa kijeshi na Ufaransa.

Vikosi vya ECOWAS katika moja ya misheni ya mwisho ya kijeshi, katika mji mkuu wa Gambia Banjul, Januari 22, 2017.
Vikosi vya ECOWAS katika moja ya misheni ya mwisho ya kijeshi, katika mji mkuu wa Gambia Banjul, Januari 22, 2017. © Jérôme Delay / AP
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi jioni, katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni, viongozi wa mapinduzi walishutumu "mikataba ya ushirikiano katika nyanja ya usalama na ulinzi na Ufaransa", ambayo kikosi chake cha kijeshi cha wanajeshi 1,500 kimetumwa nchini Niger kwa mapambano dhidi ya ugaidi katika nchi hii inayokumbwa na vurugu za wanajihadi.

Usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ambao ulikuja kutafuta suluhisho la kidiplomasia la mgogoro huo, uliondoka Niamey, bila kukutana na mkuu wa utawala wa kijshi, Jenerali Abdourahamane Tiani, pamoja na rais Mohamed Bazoum, aliyetimuliwa mamlakani. Kutofaulu huku kunatokea siku mbili kabla ya tarehe ya mwisho iliyotolewa na jumuiya ya kikanda kuhusu kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba.

ECOWAS, ambayo iliweka vikwazo vizito kwa Niamey, ilitoa makataa kwa viongozi wa mapinduzi hadi Jumapili kumrejesha mamalakani rais Mohamed Bazoum, ambaye alipinduliwa Julai 26, kwenye wadhifa wake, la sivyo itatumia "nguvu". Mkutano wa wakuu wa ECOWAS ulikamilika Ijumaa alasiri huko Abuja, wakati majeshi kadhaa ya Afrika Magharibi, likiwemo lile la Senegal, yanasema wako tayari kutuma wanajeshi ikiwa uingiliaji kati wa kijeshi utaamuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.