Pata taarifa kuu

Mgogoro nchini Niger: Algeria yaanza upatanishi katika nchi tatu za ECOWAS

Algeria, ambayo inapinga uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Niger, siku ya Jumatano imemtuma Waziri wake wa Mashauri ya Kigeni, Ahmed Attaf, katika ziara nchini Nigeria, Benin na Ghana, kusaidia kutafuta njia ya kuondokana na mzozo huo, diplomasiaya Algeria  imetangaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf mnamo Juni 22, 2023 mjini Berlin.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf mnamo Juni 22, 2023 mjini Berlin. AP - Fabian Sommer
Matangazo ya kibiashara

Waziri Ahmed Attaf, "aliyeagizwa na rais Abdelmadjid Tebboune, anaanza leo (Jumatano) ziara za kikazi nchini Nigeria, Benin, na Ghana," wizara ya mashauriano ya kigeni  ya Algeria imetangaza kwenye ukurasa  wake wa X (zamani ikiitwa Twitter).

Atafanya "mashauriano kuhusu mgogoro wa Niger na njia za kukabiliana nao" na wenzake kutoka nchi hizi "ambazo ni za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS)", imesema wizara hiyo.

Lengo ni kuchangia "katika suluhu la kisiasa ambalo litaepusha nchi hii na kanda kwa ujumla na athari za uwezekano wa kuongezeka kwa hali hiyo".

Diplomasia ya Algeria ina historia ndefu ya upatanishi au majaribio ya kusuluhisha migogoro mingi ya kimataifa.

Rais Tebboune alionyesha mnamo Agosti 6 kwamba "alikataa kabisa vikosi vya nje kuingilia kati kijeshi" nchini Niger, kitendo ambacho, ni "tishio la moja kwa moja kwa Algeria", amesema.

"Hakutakuwa na suluhu bila sisi. Sisi ndio wa kwanza kuhusika," ameongeza, wakati wa mahojiano yaliyotangazwa na televisheni ya taifa.

Algeria inashiriki karibu kilomita 1,000 za mpaka na Niger.

Taifa kubwa zaidi barani Afrika, Algeria inapakana na nchi mbili zilizo katika machafuko makubwa: Mali na Libya, na inakataa kufunguliwa kwa sehemu ya tatu kwenye mipaka yake.

Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika (AU) liliamua "kusimamisha ushiriki wa Niger katika shughuli zote za AU na vyombo vyake na taasisi zake hadi kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba nchini," kulingana na taarifa iliyotolewa Jumanne.

Baada ya kupinduliwa Julai 26 na wanajeshi wa rais wa Niger Mohamed Bazoum, aliyechaguliwa mwaka 2021, ECOWAS ilitangaza Agosti 10 nia yake ya kupeleka kikosi cha Afrika Magharibi "kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Niger".

"Nchi mbili (Mali na Burkina Faso) ziko tayari kuingia vitani (pamoja na Niger)", amesisitiza Bw. Tebboune, akikadiria kwamba katika tukio la operesheni ya kijeshi, "Sahel nzima ' itawaka moto'.

Nchini Mali na Burkina Faso, zinaokabiliwa na ghasia za wanajihadi kama Niger, viongozi wa mapinduzi katika nchi hii walionya kwamba watasimama kwa mshikamano na jirani yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.